Home Habari za michezo UTAMU WA CHAN 2024 HUU HAPA…UFUNGUZI TZ ,KWA MKAPA….ZANZIBAR NDANI…..

UTAMU WA CHAN 2024 HUU HAPA…UFUNGUZI TZ ,KWA MKAPA….ZANZIBAR NDANI…..

Habari za Michezo leo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeitangaza Tanzania kama nchi itakayoandaa mechi na tukio la ufunguzi wa fainali za CHAN 2024 zitakaofanyika kuanzia Agosti 2 hadi Agosti 30 mwaka huu katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na CAF  imeeleza kuwa hafla ya uzinduzi wa fainali hizo itafanyika Jumamosi, Agosti 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

CAF imeamua mechi ya Fainali kuchezwa katika Uwanja wa Kasarani, Kenya na mechi ya kuwania mshindi wa tatu itachezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda.

CAF pia imeipa Zanzibar uenyeji wa mechi za kundi mojawapo la fainali hizo.

“Zaidi ya hayo, Zanzibar imeteuliwa kuwa mojawapo ya Viwanja vitakavyoandaa. Uamuzi ambao unaonyesha dhamira ya CAF ya kupanua ufikiaji na ushirikishwaji wa soka la Afrika.

“Uwanja wa Amaan Zanzibar hivi karibuni ulifanikiwa kuandaa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2024/25 Mei mwaka huu,” imesema taarifa ya CAF.

Miji Wenyeji wa Hatua za Makundi za Mashindano hayo ni kama ifuatavyo:

Kundi A | Nairobi, Kenya: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia

Kundi B | Dar es Salaam, Tanzania: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kundi C | Kampala, Uganda: Uganda, Niger, Guinea, Afrika Kusini, Algeria
Kundi D | Zanzibar: Senegal, *Congo, Sudan, Nigeria.

Muda mfupi baada ya CAF kutoa taarifa hiyo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amewasihi Watanzania kutumia fursa za mashindano hayo.

“Prof. Kabudi anatoa wito kwa wadau wote kuchangamkia ipasavyo fursa mbalimbali zinazoambatana na kufanyika kwa mashindano hayo ikiwemo biashara za bidhaa mbalimbali, huduma za usafiri, utalii na kuvutia wawekezaji.

“Mashindano ya CHAN 2025 yatafuatiwa na mashindano ya AFCON 2027 ambapo Tanzania, Uganda na Kenya zitakuwa wenyeji baada ya Marais wa nchi hizo kuridhia kufanyika kwake na kuelekeza maandalizi ya miundombinu na timu za Taifa kufanyika,” imesema taarifa ya wizara.

SOMA NA HII  USAJILI WA NKANE YANGA WAZUA JAMBO...UONGOZI WAGUSIA KUTEMA MCHEZAJI...