Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUMALIZA…SIMBA WAANZA WIKI NA BIL 20 ZA BETWAY….CHUMA KIPYA...

BAADA YA YANGA KUMALIZA…SIMBA WAANZA WIKI NA BIL 20 ZA BETWAY….CHUMA KIPYA HIKI HAPA..

Habari za Simba leo

Simba imesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh20 bilioni na Kampuni ya ubashiri wa matokeo ya michezo ya Betway kama mdhamini mkuu wa klabu hiyo.

Mkataba wa udhamini huo unasainiwa leo Jumanne, Julai 29, 2025 jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ndio itakuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo kufuatia kuvunjwa kwa mkataba baina ya Simba na mdhamini mkuu aliyepita.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Zubeda Sakuru amesema kuwa udhamini huo utakuwa na faida kubwa kwa klabu hiyo.

“Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika.

“Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,” amesema Sakuru.

Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika, Jason Shielda amesema kuwa mkataba huo una maana kubwa kwa pande zote mbili.

“Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili.

“Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili,” amesema Jason.

DE REUCK MASHINE MPYA YA KAZI

RASMI Simba SC imefanya utambulisho wa mchezaji wa kwanza kuelekea msimu wa 2025/26. Hii ni baada ya sanduku la usajili kupatikana kwenye kina kirefu cha bahari ya Hindi.

Baada ya usajili kufunguliwa Simba SC ilikuwa kimya huku watani zao wa jadi wakitambulisha wachezaji wapya wa kazi kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Anaitwa Rushine De Reuck ambaye ni beki aliyewahi kucheza Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini anakotokea Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids.

Haya ni maandailizi ya Simba SC ikiwa ni kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

SOMA NA HII  BAADA YA KUINA YANGA IKITESEKA JUZI DHIDI YA NAMUNGO...KAZE ATIKISA KICHWA KISHA AFUNGUKA HAYA..