Habari za Yanga
Habari za michezo

ALLY KAMWE:- TUMETOKA LAKINI TUNA REKODI ZETU….ANAYESEMA TUMEKIMBIA AJE TUKIPIGE..

admin January 8, 2024 2:03 pm

Wakati mashabiki wa Simba wakitamba kwamba watani wao Yanga wamewakimbia kwa kukubali kipigo mbele ya APR wamejibiwa wakiambiwa leteni barua ya kuomba mechi tukipige.

Meneja Habari na Mawasiliano Yanga, Ally Kamwe amesema klabu yao imeyapokea matokeo iliyopata jana dhidi ya APR lakini hakuna ukweli kwamba wameikimbia timu yoyote kwani hakuna wanayemuogopa.

Yanga jana imepokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa APR kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyopigwa Uwanja wa New Amani Complex hapa Unguja.

Kamwe amesema Yanga inatoka ikiwa na timu yenye rekodi ya kutoa kipigo kikubwa ambacho kimekuwa maaarufu kukitoa kwa klabu mbalimbali.

Amesema kama kuna timu inaona imekimbiwa waiandikie barua mapema waombe kucheza nao kabla ya wao kuondoka Unguja kisha waonyeshane ubabe.

“Yanga inawezaje kuogopa hizi timu zingine hasa Yanga hii ya msimu huu? Mashabiki wetu watulie tumepoteza mchezo kihalali dhidi ya APR makocha wetu wamepata nafasi ya kuchukua changamoto hizo na kwenda kuzifanyia kazi na sisi tuliobaki tunapaswa kuwaachia wao,” amesema Kamwe

“Kama wapo ambao wanaona tumewakimbia basi watuandikie barua watuletee haraka kabla hatujaamua safari ya kurudi kwetu, tuonyeshane, sisi ndio timu ambayo imetoa kipigo kikubwa hapa, tena kile ambacho tuliwapiga wale jamaa,”

MCHAMBUZI;- MASTAA HAWA NDIO WAMEIANGUSHA YANGA JANA…WALISTAHILI KUFUNGWA 5.. ANAYEFUATA KUTAMBULISHWA SIMBA HUYU HAPA….TAYARI YUKO ZAKE ZNZ MAPEMA TU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “ALLY KAMWE:- TUMETOKA LAKINI TUNA REKODI ZETU….ANAYESEMA TUMEKIMBIA AJE TUKIPIGE..”

  1. philipo says:

    mh yanga yanga nyieeh mtaniua mieeh

Leave a Reply