Home Azam FC PICHA LA FEI TOTO LAENDELEA AZAM…AJILI KIAPO CHA LAZIMA KUHUSU HATMA YAKE…

PICHA LA FEI TOTO LAENDELEA AZAM…AJILI KIAPO CHA LAZIMA KUHUSU HATMA YAKE…

habari za simba

AZAM FC tayari ipo Juba, Sudan Kusini kwa ajili ya mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao, El Merrikh Bentiu, huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akila kiapo wamefuata ushindi ili kujiweka pazuri.

Wawakilishi hao wa Tanzania watashuka uwanjani Jumamosi ya wiki hii kuumana na wenyeji wao hao katika mechi ya mkondo wa kwanza, huku Fei Toto akisema wamejiandaa kuipambania timu kwa lengo la kufikia malengo kwa msimu huu itinge makundi ya CAF kwa mara ya kwanza.

Akizungumza Fei Toto ambaye msimu uliopita akiwa na kikosi hicho waling’oa raundi ya kwanza kwa kutolewa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 2-1, alisema maandalizi kwa upande wao yanaendelea vizuri na wapo tayari kuonyesha ushindani mbele ya wenyeji.

“Kwa jumla maandalizi hadi sasa yanaenda vizuri na kama wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunaipambania timu yetu inaanza vizuri mchezo huu wa raundi ya kwanza kwa kupata matokeo na kucheza hatua inayofuata,” alisema Fei aliyeongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja hadi 2017.

“Hatutarajii mechi rahisi kila mmoja anatambua ugumu ulio mbele yetu, hivyo utayari unahitajika ili tuweze kufanya vitu kwa usahihi na kutinga hatua inayofuata kama malengo ya benchi uongozi na wachezaji tulivyojiwekea,” aliongeza Fei Toto aliyemaliza kama kinara wa asisti katikia Ligi Kuu msimu uliopita mbali na kufunga mabao manne yaliyouifanya Azam imalize ya tatu.

Fei Toto alisema Jumamosi, wataingia kwa kuwaheshimu wenyeji, lakini akili yao ikiwa tayari kwa kupambania nembo ya klabu na kuweka wazi ubora wa benchi la ufundi na uzoefu wa baadhi ya wachezaji itakuwa chachu ya wao kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

“Hakuna mchezo rahisi timu hati inapata nafasi ya kuiwakilisha nchi yake kwenye michuano hii imefanya kazi kubwa hivyo hatutarajii wepesi tunajiandaa kwenda kushindana na maandalizi kwa jumla yanakwenda vizuri.”

Mara baada ya mechi hiyo ya wikiendi hii, timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam Septemba 28 kwenye Uwanja wa Azam Complex na mshindi wa jumla atatinga raundi ya pili kucheza na mshindi wa mechi kati ya KMKM ya Zanzibar na AS Port ya Djibouti.

SOMA NA HII  SIMBA KUINGIZA MIL 2.2 KILA SEKUNDE 60...MO DEWJI AFANYA MAAJABU YAKE...JASHO NA DAMU KWA MKAPA