Home Habari za michezo HUYU HAPA MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA GOLI LIGI KUU MSIMU HUU 2025/26…

HUYU HAPA MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA GOLI LIGI KUU MSIMU HUU 2025/26…

Ligi Kuu Tanzania 2023/24

DARUWESH Saliboko wa KMC amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga bao katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 alipoiwezesha timu hiyo kuibuka washindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji ameanza mbwembwe mapemaa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Polisi Tanzania na Lipuli, alisema ushindi iliyopata KMC ikiwa nyumbani ulikuwa ni mpango wa timu na benchi la ufundi na amefuraha kuwa nyota wa kwanza kufunga bao msimu huu.

Saliboko amefunga bao dakika ya 56 akimalizia pasi ya Rashid Chambo akiipa KMC pointi tatu za kwanza katika Ligi Kuu iliyoanza rasmi aliliambia Mwanaspoti, haikuwa rahisi lakini anajisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi hicho dhidi ya Dodoma Jiji.

Alisema furaha hii imetokana na ukweli Dodoma imekuwa ni moja ya timu inayoitesa KMC kila zinapokutana na ushindi huo ni faraja kwao, kwani katika mechi 11 walizovaana katika Ligi Kuu, Dodoma imeshinda mara saba na Wana Kinondoni wakitamba mara nne ikiwamo hiyo ya juzi.

“Nafasi ya kufunga imechangiwa na timu nzima sambamba na benchi la ufundi baada ya kukosa nafasi ya kufanya hivyo kipindi cha kwanza kocha alinipa maelekezo wapi nipite ili kuipa matokeo timu,” alisema Saliboko na kuongeza;

“Mchezo ulikuwa mgumu na wa ushindani ni kawaida kila tunapokutana na Dodoma Jiji kwani huwa mchezo unakuwa mgumu na hii timu imekuwa ikitufunga sana msimu huu hatujataka kufanya makosa.”

Saliboko alisema huo ni mwanzo kwa timu yao kupata matokeo mpango wao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye kila mchezo ili tuweze kufikia malengo.

“Ushindi tulioupata unaongeza morali kwa timu kuhakikisha tunaendeleza morali tuliyoipata kwa kupata matokeo zaidi kwenye mechi zilizobaki hasa kwenye uwanja wetu wa nyumbani.”

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA WANAWAKE KESHO....SIMBA QUEENS WAIPIGA MKWARA WA KUFA MTU YANGA PRINCESS...