Home Habari za michezo HIZI HAPA DK 270 ZIJAZO ZA FOLZ KUJITETEA NDANI YA YANGA….AKIZINGUA HAPA...

HIZI HAPA DK 270 ZIJAZO ZA FOLZ KUJITETEA NDANI YA YANGA….AKIZINGUA HAPA ANASEPESHWA…

Habari za yanga leo

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 Yanga SC wana dakika 270 za kazi ndani ya Oktoba kwa mechi tatu za ushindani uwanjani.

Hizo ni mechi tatu za kazi kwa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi sita bila kuambulia kipigo.

Kwenye mechi hizo sita, tano Folz alishuhudia Yanga SC ikishinda na mechi moja walitoshana nguvu ilikuwa dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 30 2025.

Katika mechi hizo tatu, watacheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi mchezo wa kwanza itakuwa ugenini Malawi kati ya tarehe 17-19 na ule wa marudiano utapigwa nyumbani kati ya tarehe 24-26.

Mchezo mmoja ni wa ligi ya NBC itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar Oktoba 29 2025 Uwanja wa Mkapa katika msako wa pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  YANGA YATOA SIRI NZITO USAJILI WA MUSONDA...ULE NI USAJILI WA KIMKAKATI