Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI IJAYO MALI….PANTEV ATAJA MIPANGO MIPYA SIMBA…MASTAA TUMBO JOTO…

KUELEKEA MECHI IJAYO MALI….PANTEV ATAJA MIPANGO MIPYA SIMBA…MASTAA TUMBO JOTO…

Habari za Simba leo

KIKOSI cha Simba tayari kimeshatua Mali kwa ajili ya mechi y pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien, lakini wakati kinaanza safari kuna hesabu amezitoa meneja wa timu hiyo, Dimitar Pantev, akiweka bayana kwamba ana mipango mipya ugenini na kutahadharisha mastaa.

Iko hivi. Baada ya Simba kupoteza nyumbani katika mechi ya kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Petro Atletico, lawama zote ziliangushwa kwa Pantev kutokana na kutoanza na mshambuliaji asilia wa kati na jamaa huyo amekubali akisema presha ni sehemu ya maisha ya ukocha na bado ana imani.

Akizungumza kabla ya kuondoka nchini, Pantev alisema anajua wapi wachezaji walikosea licha ya kutengeneza nafasi, lakini amekaa nao na kuwapa akili namna ya kutengeneza utulivu na warudi kushinda mechi hiyo ya pili ya Kundi D inayochezwa Jumapili Stade 26 Mars, jijini Bamako.

Pantev alisema anaamini wachezaji wamejua wapi walikosea na wamewasoma wapinzani wao wa Jumapili na kwamba kitu kitakachowaondolea presha ni kushinda mechi hiyo.

“Tulikosa matokeo mazuri katika mechi iliyopita na inatokea kwenye soka, tulitengeneza nafasi za wazi kuliko hata hiyo moja ambayo wenzetu waliitumia, kosa letu ni kwamba hatukutumia tulichokitengeneza,” alisema Pantev na kuongeza;

“Tunatakiwa kusahau hilo na kulichukua kama funzo, nimeongea na wachezaji na kuwapa akili ya namna wanavyotakiwa kutulia, hatutakiwi kufanya mambo kwa presha, tunaweza kushinda mchezo ujao tuna timu nzuri na maandalizi mazuri.”

Akizungumzia mabadiliko Pantev alisema kunaweza kukawa na mabadiliko machache ya namna ya muundo wa kikosi hicho kulingana na wapinzani anaokwenda kukutana nao, ila watakwenda kutafuta ushindi.

“Mabadiliko yanaweza kuwapo tunakwenda kukutana na mpinzani mgumu mwingine akiwa kwake, sio rahisi sana kushinda ugenini, lakini tutakwenda kujaribu kufanya hivyo tena, tunaweza kubadili baadhi ya mambo kwenye kikosi kila mechi ina mahesabu yake,” alisema Pantev na kuongeza;

“Tutaangalia ni wachezaji gani bora tunaweza kuwatumia, tutaondoka na wachezaji 21 ambao watakuwa tayari kwa mchezo huu, tunaweza pia kubadilika kwa mbinu, kitu muhimu hapa ni kutumia ubora wetu kubadilisha matokeo.”

SOMA NA HII  KOCHA TAIFA STARS:- HAKUNA SABABU YA KUSINGIZIA...TUTAWAPA FURAHA WATANZANIA