Home Habari za michezo BAADA YA KUWAPIGA BAO SIMBA CAF….UELEKEO WA YANGA HUU HAPA….KOCHA ATIA NDIMU…

BAADA YA KUWAPIGA BAO SIMBA CAF….UELEKEO WA YANGA HUU HAPA….KOCHA ATIA NDIMU…

Habari za Yanga leo

MASHABIKI wa Yanga wana furaha vilevile mabosi wao, siri ni moja tu ni kwamba kikosi cha timu hiyo kilivyobadilika, lakini kocha Pedro Goncalves mwenyewe humwambii kitu kuhusu wachezaji.

Kocha Pedro amesema kuwa amekielewa kikosi cha timu hiyo na kwamba sasa ana imani kubwa na wachezaji namna wanavyoendelea kuimarika kwenye mechi ambazo amekuwa nao hadi sasa.

Pedro alisema kwa ujumla ameridhika na wachezaji namna wanavyoonyesha wana njaa ya mafanikio, wakionyesha uthubutu wakitaka kujitambulisha kwamba hata wao wanastahili heshima mbele ya timu zenye historia kubwa.

Kocha huyo Mreno alisema kwa kiwango ambacho wachezaji wamekionyesha katika mechi mbili za makundi dhidi ya klabu mbili za Afrika Kaskazini, kitazifanya nyingine kuja kwa heshima na sio kuwadharau.

“Navutiwa sana na namna wachezaji wangu wanavyoimarika, ukiwa kocha katika timu kama hii halafu ukaona namna wachezaji wako wanavyopambana dhidi ya timu zenye historia kubwa huku wakionyesha wana njaa ya mafanikio, inakupa nguvu kubwa kocha, kiukweli nina furaha sana na wachezaji nilionao hapa,” alisema Pedro na kuongeza;

“Napenda kuona wanavyoshindana kuanzia mazoezini inavutia kuona wachezaji wanahitaji sana matokeo mazuri, tumekutana na timu mbili za kutoka Afrika Kaskazini, watu waliona kama haitawezekana, tutapoteza vibaya lakini tumeonyesha tunastahili heshima yenye usawa.

“Tunaweza kuwa bora zaidi kama tutaendelea kutamani hatua kubwa zaidi ya hiki ambacho tumeonyesha, jambo zuri zaidi hapa tunafanya kazi kwa ukaribu sana na viongozi na mashabiki wetu wako nyuma yetu wakati wote.”

Aidha, Pedro aliongeza kwa sasa wanarudi kuangalia mechi za ratiba ya Ligi Kuu Bara, huku wakipiga hesabu za mechi nne zilizosalia hatua ya makundi ili Yanga iendelee kutafuta ushindi mwingine utakaowaweka eneo zuri kwenye kundi lao.

“Akili yetu sasa ni mechi za ligi ya ndani, kisha tunajipanga kuangalia tutarudije katika mashindano ya CAF.”

“Tuna pointi nne lakini nimewaambia wachezaji wangu kwamba, hatutakiwi kuridhika tunaweza kushinda zaidi, tunatakiwa kuweka mikakati ya kushinda mechi zilizosalia bila kujali tunakutana na timu ipi, kitu muhimu ni kuheshimu mpinzani na kucheza kwa mkakati wetu.”

SOMA NA HII  LUNYAMILA: KWA HILI LA NAMUNGO, TFF WANASTAHILI PONGEZI