Home Habari za michezo MTANZANIA APEWA MWAKA MMOJA NA NUSU

MTANZANIA APEWA MWAKA MMOJA NA NUSU

17
0

MSHAMBULIAJI wa Kitanzania, Oscar Evalisto amejiunga na Port Fouad inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Makadi FC.

Evalisto aliitumikia Makadi kwa msimu mmoja akifunga mabao matano na asisti nne kwenye mechi 10 alizocheza akiibuka na tuzo moja  ya mchezaji bora wa mwezi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Evalisto amesema Port walitaka kumpatia mkataba wa miaka mitatu lakini alisaini mwaka mmoja na nusu ili aweze kusikilizia ofa za timu za Ligi Kuu.

“Nina siku nne tangu nimejiunga hapa, timu inacheza Ligi Daraja la Pili lakini inataka kupanda daraja la kwanza na inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne, kesho tuna mechi na timu inayotufuatia kwa pointi.

“Nataka nipambane nimalizie hii miezi sita kama itapanda hii timu itakuwa vizuri zaidi ili msimu ujao nicheze daraja la kwanza kwa kumalizia tu msimu halafu nione hizo baadhi ya timu zinazonifuatilia za ligi kuu tutakuwa tumefikia wapi,” amesema.

“Malengo yangu ni kucheza ligi kuu na kuna timu ambazo tayari zinanifuatilia kupitia hii timu mpya kwa maana hii timu haipo mbali na mjini, kwa hiyo itakuwa rahisi wao kunifuatilia kwa ukaribu tofauti na ile timu ya mwanzo ilikuwa mbali sana.”