Home Habari za michezo WINGA WA SIMBA UARABUNI

WINGA WA SIMBA UARABUNI

224
0

SIKU chache tu tangu winga wa Simba, Edwin Balua kuondoka Enosis Neon Paralimniou inayoshiriki Ligi Kuu Cyprus ikiwa na maskani katika Jiji la Paralimni aliyoitumikia kwa mkopo, kwa nyota huyo ameibukia Uarabuni kujiunga na Al-Entesar ya Saudi Arabia.

Balua anayemudu kucheza winga zote kulia na kushoto huku akicheza pia nyuma ya mshambuliaji, tayari amekamilisha uhamisho huo ikiwa ni baada ya kuitumikia Enosis Neon Paralimniou tangu Agosti 20, 2025.

Nyota huyo alijiunga na timu hiyo kwa mkopo baada ya kupata dili hilo, ambapo kwa sasa amesaini tena kuichezea Al-Entesar yenye makazi Rabigh, Saudi Arabia, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

Al-Entesar iliyoanzishwa 1978, ni timu inayojulikana zaidi ambapo hushiriki mara kwa mara katika Ligi Daraja la Pili, ambayo ni ngazi ya tatu katika mfumo wa ligi za mpira wa miguu zinazochezwa nchini humo.

Balua alijiunga Simba katika dirisha dogo la Januari 2024 akitokea Tanzania Prisons ambapo msimu wa 2023-2024, alimaliza na mabao manne Ligi Kuu Bara, huku akizifungia mawili kwa kila moja kati ya hizo.

Ndani ya msimu wa 2024-2025 kabla ya kwenda Cyprus aliifungia Simba mabao mawili Ligi Kuu, huku bao lake la mwisho likiwa la ushindi wa 4-0 dhidi ya KMC mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Novemba 6, 2024.