Home Habari za michezo TOURE AAGA BANIYAS, AJIANDAA KUVAA JEZI MSIMBAZI

TOURE AAGA BANIYAS, AJIANDAA KUVAA JEZI MSIMBAZI

3325
0

BEKI  wa kati wa klabu ya FC Baniyas inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE), Ismael Oliver Touré, ameaga rasmi klabu hiyo na sasa anatajwa kuwa karibu kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC, katika dirisha la usajili.

Touré amekuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa katika klabu mbalimbali alizopita, ikiwemo Stellenbosch FC, ambako aliwahi kuwa nguzo muhimu chini ya kocha mkuu Steve Barker, kabla ya kwenda kujaribu changamoto mpya katika soka la Falme za Kiarabu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, beki huyo alithibitisha kuondoka kwake Baniyas kwa ujumbe mzito wa shukrani, akieleza kuwa imekuwa vigumu kwake kupata maneno sahihi ya kuaga klabu iliyokuwa kama familia kwake.

Amesema  kipindi chake ndani ya Baniyas kilikuwa cha kipekee na chenye kumbukumbu nyingi, huku akiwashukuru wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na mashabiki kwa sapoti kubwa aliyopata.

Touré ameongeza kuwa licha ya kuanza safari mpya, ataendelea kubeba kumbukumbu zote alizozijenga akiwa na Baniyas, amejifunza mambo mengi ndani ya klabu hiyo na akaiahidi kuendelea kufuatilia matokeo yao hata baada ya kuondoka.

Katika ujumbe wake, nyota huyo aliwashukuru pia wachezaji wenzake kwa kumsaidia kuinua kiwango chake kila siku, huku akiwapongeza mashabiki kwa sapoti yao isiyo na kifani.

Amesisitiza  kuwa ukurasa mpya uko mbioni kufunguliwa katika maisha yake ya soka, lakini heshima na mapenzi yake kwa Baniyas yataendelea kuwepo.

Touré amesema  kwa kusema anaondoka akiwa na furaha na heshima kubwa kwa klabu hiyo, kuwa njia zao zinaweza kukutana tena siku za usoni ndani ya ulimwengu wa soka, huku sasa macho yakielekezwa kwenye uwezekano wa kuanza rasmi safari mpya ndani ya kikosi cha Simba SC.