Home Habari za michezo MFUMO WA YANGA WAANZA KUELEWEKA

MFUMO WA YANGA WAANZA KUELEWEKA

141
0

KOCHA Mkuu  wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema kikosi chake kimeanza kuonyesha mabadiliko chanya baada ya wachezaji wapya kuelewa kwa kina falsafa na mahitaji yake ndani ya uwanja.

Pedro amesema hali hiyo imeongeza ufanisi wa timu na kufanya mawasiliano kati ya benchi la ufundi na wachezaji kuwa rahisi zaidi kuliko awali.

Ameeleza kuwa mwanzoni haikuwa rahisi kwa wachezaji kuzoea mfumo wake kutokana na mabadiliko ya mbinu na majukumu mbalimbali aliyoweka.

“Kadri muda ulivyopita na kupitia mazoezi ya mara kwa mara, wachezaji wameanza kuuelewa mfumo huo na kuutekeleza kwa ufanisi mkubwa wakati wa mechi.

maendeleo hayo yamechangia pia kuwapa nafasi nzuri wachezaji wapya kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa timu bila changamoto kubwa,” amesema.

Pedro amesema wachezaji wapya hawachukui muda mrefu kuzoea kwa sababu wanakuta mfumo tayari unaeleweka na unatekelezwa na kila mmoja.

Akizungumzia matumizi ya wachezaji wapya, Pedro amesema siri kubwa ya mafanikio yao ni kuhakikisha kila mchezaji anatumika kwenye nafasi anayoiweza zaidi.

Amefafanua kuwa falsafa yake ni “kuweka wachezaji sahihi kwenye nafasi sahihi ili kuongeza ubora wa timu kwa ujumla,”.

Pedro ameongeza kuwa njia hiyo inasaidia pia kupunguza presha kwa wachezaji wapya, wanapocheza kwenye nafasi wanazozoea, wanakuwa na ujasiri na uwezo mkubwa wa kuonyesha viwango vyao halisi .

“Kuifanya Yanga kuwa timu yenye ushindani mkubwa katika kila mchezo,  lengo lake ni kujenga timu imara yenye mtiririko mzuri wa uchezaji na matokeo chanya,” amesema.