Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUSAJILIWA SIMBA….AHMED ALLY ‘ATUPA JIWE GIZANI’ KWA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUSAJILIWA SIMBA….AHMED ALLY ‘ATUPA JIWE GIZANI’ KWA KIBABAGE…

302
0
Kibabage Simba

MSEMAJI wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kumpokea na kumpa ushirikiano beki wa kushoto Nikson Kibabage, akisisitiza kuwa ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kuisaidia timu.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo, Ahmed amesema Kibabage ana ubora na uwezo ambao, endapo atapewa sapoti inayostahili, ataifanyia makubwa Simba.

“Tumpokee kijana wetu, tumpe ushirikiano. Kwa uwezo na ubora alikuwa nao, atatufanyia makubwa sana ndani ya timu yetu,” alisema Ahmed Ally.

Nikson Kibabage alitambulishwa rasmi jana kama mchezaji mpya wa Simba SC, baada ya kusajiliwa katika dirisha hili la usajili akitokea Singida Black Stars, akijiunga na kikosi hicho chenye rekodi kubwa ndani ya soka la Tanzania.

Usajili wa Kibabage unaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa Simba wa kuziba pengo la beki wa kushoto lililoachwa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ aliyejiunga na Yanga SC tangu mwanzoni mwa msimu huu, nafasi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haijapata mrithi wa kudumu.