STRAIKA wa Pyramids ya Misri na timu ya taifa ya DR Congo, Fiston Mayele, ameonyesha wazi furaha yake baada ya Clatous Chama, kurejea katika klabu ya Simba.
Kupitia sehemu ya maoni mitandaoni baada ya Simba kutangaza kumrejesha Chama, Mayele aliandika ujumbe uliovuta hisia za mashabiki wengi huku wengine wakitaka naye atue Msimbazi.
βThe Best Number 10 Is Back, Mwamba wa Lusaka good luck!,β amekomenti Mayele katika chapisho la Simba kwenye instagram wakati ikimtambulisha Chama akiwa na maana ya kwamba namba kumi bora amerejea kisha akamtakia kila la kheri.
Baadhi ya waliochangia katika komenti ya Mayele kuhusu usajili huo wa Chama wameandika maoni mbalimbali wakimtaka mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara 2022β23 na Mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Afrika 2022β2023 wakati anaichezea Yanga, atue Simba akitokea Pyramids.
“Bado wewe”
“Sasa mpaka Mayele anamkubali daaah ila chama π₯ππ₯”
“Ungekuja wewe mimi ningefurahi sana hapa Simba yani mambo yangekuwa mazuri sana.”
“Bado wewe tunakusubiri.”
“Rudi kaka utusaidie Wanasimba hatuelewi.”
“Tunakusubiri na wewe Mzee wa kutetema uje Unyamani.”
Ujumbe huo umeonyesha heshima kubwa kwa Chama, ambaye ni mmoja wa viungo mahiri waliowahi kuichezea Simba na kuacha alama kubwa katika Ligi Kuu ya Tanzania.
Mbali na Chama, mastaa wengine walioonyesha hisia zao juu ya usajili huo ni kiungo wa zamani wa Yanga anayecheza Singida Black Stars, Khalid Aucho aliyeandika ujumbe wa kumpongeza na kumtakia kila la kheri: “Congratulations brother and good luck ππππβ€οΈβ€οΈ.”
Naye mshambuliaji wa zamani wa Simba na Namungo, Meddie Kagere ameandika ujumbe wa kumkaribisha: “Welcome back @realclatouschama.”
Wakati huohuo, kiungo wa zamani wa Simba, Pape Ousmane Sakho, naye amendika: “Wow wow wowπ₯π₯ @realclatouschama.”
Winga wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi naye ameandika: “Karibu tena nyumbani @realclatouschama.”
Huku beki wa zamani wa Simba na Azam, Pascal Wawa amemkaribisha Chama kwa kuandika: “Welcome back home capitaine Mario.”
Kwa sasa, Chama ni Mnyama tena, na mashabiki wa Simba wanaamini kurejea kwake ni baraka kubwa kwa klabu hiyo kuelekea mapambano yao ya msimu huu.