Home Habari za michezo SIMBA SULEIMAN AKARIBISHWA, NANGU AFRIKA KUSINI

SIMBA SULEIMAN AKARIBISHWA, NANGU AFRIKA KUSINI

0

BEKI wa Simba SC, Wilson Nangu, anatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini mwishoni mwa wiki kwa ajili ya matibabu ya kifundo cha mguu ambacho kinahitaji upasuaji.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema hali ya wachezaji wengi wa timu inaendelea kuwa shwari, ingawa kuna wasiwasi kidogo kuhusu mshambuliaji huyo.

Amesema wachezaji wengi wanapata maendeleo chanya katika mazoezi na mechi za hivi karibuni, jambo ambalo linampa kocha Steve Barker matumaini makubwa kuelekea michezo ijayo.

“Nangu amepata majeraha ya kifundo cha mguu ambayo yanahitaji upasuaji. Atapelekwa Afrika Kusini mwishoni mwa wiki kwa matibabu haya,” amesema Ahmed.

Amesema upasuaji huo unatarajiwa kumsaidia Nangu kurejea kwenye kiwango chake cha juu bila hatari ya kuumia tena, kuwa baada ya upasuaji kufanyika, timu itakuwa na taswira kamili ya muda atakaohitaji Nangu kurudi kikosini.

Kwa upande mwingine, maendeleo ya kipa wa Simba, Yakubu Suleiman, yameendelea vizuri,anaweza kurejea kikosini muda wowote, jambo linaloongeza nguvu zaidi kwenye kikosi cha Simba kabla ya mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Steve Barker ana matumaini makubwa kuwa kurejea kwa Suleiman pamoja na matibabu ya Nangu kutasaidia timu kuwa na kikosi kamili, tayari kukabiliana na changamoto zote za msimu huu.