Home Habari za michezo DAKIKA 90 ZAMFANYA BARKER AIBUE SIRI ZA YANGA KABLA YA KARIAKOO DABI

DAKIKA 90 ZAMFANYA BARKER AIBUE SIRI ZA YANGA KABLA YA KARIAKOO DABI

0

KKOCHA  Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameanza maandalizi ya kina kuelekea michezo miwili mikubwa ijayo baada ya kutumia dakika 90 kuisoma Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Azam FC, uliochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Barker alitumia mechi hiyo kama fursa muhimu ya kuchambua mbinu, mifumo ya uchezaji pamoja na ubora na mapungufu ya wapinzani wake, akilenga kupata picha halisi ya namna ya kukabiliana nao. Mbali na kujiandaa kwa fainali ya michuano hiyo, pia macho yake yapo kwenye Kariakoo Derby inayotarajiwa kupigwa Mei 3, 2026.

Akiwa sambamba na benchi lake la ufundi, kocha huyo ameonekana kuwa makini kufuatilia kila undani wa mchezo huo, akihakikisha hakuna kinachomponyoka katika tathmini ya wapinzani wake. Lengo kubwa ni kuja na mkakati madhubuti utakaoisaidia Simba kufanya vizuri katika mechi zijazo.

Wakati huo huo, Simba ina kibarua kingine muhimu kesho itakaposhuka dimbani kuivaa Mlandege SC katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakaopigwa Uwanja wa Amaan Complex. Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa Wekundu wa Msimbazi katika safari yao ya kusaka tiketi ya fainali.

Mshindi wa pambano hilo atakutana na Yanga tayari kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano, baada ya watani hao kufanikiwa kuitoa Azam FC na kujihakikishia nafasi hiyo.

Huku akijiandaa kwa hatua hiyo ya mwisho ya michuano, Barker pia anaendelea kukinoa kikosi chake kwa ajili ya Kariakoo Derby itakayochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, ambapo ushindani mkubwa unatarajiwa kushuhudiwa. Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Azam FC, uliochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Barker alitumia mechi hiyo kama fursa muhimu ya kuchambua mbinu, mifumo ya uchezaji pamoja na ubora na mapungufu ya wapinzani wake, akilenga kupata picha halisi ya namna ya kukabiliana nao. Mbali na kujiandaa kwa fainali ya michuano hiyo, pia macho yake yapo kwenye Kariakoo Derby inayotarajiwa kupigwa Mei 3, 2026.

Akiwa sambamba na benchi lake la ufundi, kocha huyo ameonekana kuwa makini kufuatilia kila undani wa mchezo huo, akihakikisha hakuna kinachomponyoka katika tathmini ya wapinzani wake. Lengo kubwa ni kuja na mkakati madhubuti utakaoisaidia Simba kufanya vizuri katika mechi zijazo.

Wakati huo huo, Simba ina kibarua kingine muhimu kesho itakaposhuka dimbani kuivaa Mlandege SC katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakaopigwa Uwanja wa Amaan Complex. Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa Wekundu wa Msimbazi katika safari yao ya kusaka tiketi ya fainali.

Mshindi wa pambano hilo atakutana na Yanga tayari kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano, baada ya watani hao kufanikiwa kuitoa Azam FC na kujihakikishia nafasi hiyo.

Huku akijiandaa kwa hatua hiyo ya mwisho ya michuano, Barker pia anaendelea kukinoa kikosi chake kwa ajili ya Kariakoo Derby itakayochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, ambapo ushindani mkubwa unatarajiwa kushuhudiwa.