Home Habari za michezo YANGA SI YA SIKU MOJA, ARAFAT AIBUKA NA KAULI NZITO

YANGA SI YA SIKU MOJA, ARAFAT AIBUKA NA KAULI NZITO

0

MAKAMU wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amewatuliza mashabiki wa Yanga kufuatia mabadiliko yaliyojitokeza ndani ya benchi la ufundi, amesitiza kuwa bado timu hiyo ipo kwenye njia sahihi ya kupigania malengo yake makubwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Arafat amesema soka lina nyakati tofauti zikiwemo za changamoto na mafanikio, mashabiki wanapaswa kuendelea kuwa na imani na timu yao badala ya kukata tamaa kutokana na hali ya sasa.

Kiongozi huyo ameleza kuwa kuondoka kwa Kocha Pendo Goncalves na mabadiliko yaliyofanyika kwenye benchi la ufundi si mwisho wa safari ya Yanga, bali ni sehemu ya mchakato wa kuijenga timu imara zaidi kuelekea mwisho wa msimu.

Arafat amesema Yanga ni taasisi kubwa ambayo hupimwa zaidi katika nyakati ngumu kuliko wakati wa mafanikio, akiwataka Wanayanga kuonyesha mshikamano na kuendelea kuiunga mkono timu yao katika kila hatua.

Amesisitiza kuwa bado wana michezo tisa muhimu ya Ligi Kuu Tanzania Bara mbele yao, lengo kuu likiwa ni kutetea ubingwa wa ligi pamoja na kupambana kutwaa Kombe la Shirikisho.

โ€œTunataka kuendelea kuthibitisha kuwa Yanga si klabu ya kushiriki tu, bali ni klabu ya kushindania mataji,โ€ amesema Arafat.

Arafat amewataka Wanayanga kupuuza kelele za nje na kuendelea kuwa kitu kimoja kwa ajili ya mafanikio ya timu, akisisitiza kuwa Yanga ni kubwa kuliko matokeo ya siku moja