Msimu huu Mtibwa imecheza mechi 21 za Ligi Kuu Bara, ikishinda tano, sare nane na kupoteza nane, ikifunga mabao 16 na kuruhusu 25, ikiwa nafasi ya 11 na pointi 23 kwenye msimamo.
Kocha huyo aliyewahi kuzifundisha Pamba Jiji, Coastal Union na TRA United, anakumbukwa na mashabiki wengi hasa baada ya kukiongoza kikosi cha Ulinzi Stars kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Kenya ‘KPL’ kati ya 2003 na 2005 na kuhudumu akiwa kocha msaidizi wa Harambee Stars kuanzia 2008 hadi 2011.