Licha ya changamoto za mitandaoni, Priscilla alisema familia ya mume wake walimpokea vizuri na anajihisi kuwa zaidi ya nyumbani licha ya ugeni wake.
“Nadhani familia nzima ni watu wazuri na watulivu na wamekuwa wakitusaidia sana,” alisema Priscilla akionyesha kuridhishwa na namna alivyopokelewa kwenye familia ya msanii huyo anayetamba na kibao cha ‘Joy’ alichoshirikishwa na Diamond Platnumz.
MITANDAONI
Kuhus maneno ya wanaomsema vibaya mitandao, Priscilla amekiri mara nyingi watu wanakuwa na maneno ya kashfa au chuki, lakini amechagua kutowapa kipaumbele.
Aliongeza moja ya vitu vinavyomsaidia ni kutoielewa vizuri lugha ya Kiswahili inayotumika na baadhi ya watu kumshambulia na hapendi kuangalia nini kinasemwa.
“Sitaki kujihusisha kabisa na mambo ya kutafsiri kwa sababu huwa naona maoni ya Watanzania lakini sitafsiri kwa sababu hata nikijua mengine yanaweza kuniumiza hivyo, naacha tu.”