Habari za michezo

CORAZONE ATAMANI TENA KIMATAIFA

Vardo May 10, 2026 5:56 pm

KIUNGO wa Simba Queens, Vivian Corazone amesema malengo yake msimu huu ni kubeba Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake ili arejee kucheza michuano ya Afrika.

Simba Queens inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 43 baada ya mechi 15, ikifuatiwa na Yanga Princess wenye pointi 39 na JKT Queens ya tatu na pointi 38, hali inayozidi kuongeza presha ya ubingwa kwa vigogo hao watatu.

Akizungumzia hilo, Corazone amesema msimu uliopita hawakucheza mashindano ya kimataifa akiamini kwa mwenendo wa sasa wa timu wana nafasi kubwa ya kuchukua taji hilo linalotetewa na JKT.

“Matamanio ni kubeba taji la ligi na turejee kwenye michuano ya Afrika kwa sababu tumekuwa tukicheza mara kwa mara, hivyo naamini msimu huu tutarejesha heshima yetu,” amesema Corazone.

Amesema Simba ni timu kubwa na ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi yake, hivyo kila nafasi anayopata ni lazima ipiganiwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha malengo ya klabu yanafikiwa.

“Simba ni timu kubwa na ni ndoto ya kila mchezaji kucheza hivyo tunavyopata nafasi basi nahakikisha napambania nafasi hiyo na kutetea jezi hiyo.”

Huu ni msimu wa tano kwa kiungo huyo kuitumikia Simba tangu alipojiunga nayo msimu wa 2021/22 akitokea Gaspo Women FC ya kwao Kenya.

Mkenya huyo aliifikisha Simba nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mbaingwa Afrika msimu wa 2022/23 na kuipa ubingwa wa ligi mara mbili.

MYNACO AFICHUA USHINDANI YANGA PRINCESS DODOMA JIJI WAPEWE TAHADHARI, MPIGA SIMU WA YANGA AMERUDI