Habari za michezo

NEYMAR NDANI YA BRAZIL, GYOKERES SWEDEN

Vardo May 14, 2026 10:19 am

BRASILIA, BRAZIL: HATIMAYE Neymar Jr amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifacha mastaa 55, huku nchi mbalimbali zikianza kutangaza vikosi vya awali kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026, wakati mastraika wa Arsenal, Viktor Gyokeres na mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak wakiitwa Sweden.

Hamasa inaendelea kuongezeka kuelekea michuano hiyo mikubwa itakayofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11. Ikiwa na mataifa 48, hizo zitakuwa fainali za Kombe la Dunia kubwa zaidi katika historia.

Neymar mwenye umri wa miaka 34 alikuwa kwenye shaka kutokana na matatizo ya kiwango akiwa na timu yake ya Santos msimu huu, lakini bado anaweza kuisaidia Brazil ya Carlo Ancelotti katika harakati za kusaka ubingwa wa sita wa Kombe la Dunia.

Kikosi cha Sweden kinamjumuisha mshambuliaji wa Arsenal Viktor Gyokeres pamoja na mshambuliaji wa Liverpool Alexander Isak. Hata hivyo, nyota wa Tottenham Hotspur, Dejan Kulusevski amekosekana baada ya kutocheza kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na jeraha la goti.

Vikosi hivyo vya awali vitapunguzwa hadi orodha ya mwisho ya wachezaji kati ya 23 hadi 26 kwa kila taifa, ambayo lazima iwasilishwe Fifa ifikapo Juni 1.

BOSNIA-HERZEGOVINA

MAKIPA: Nikola Vasilj (St Pauli), Martin Zlomislic (Rijeka), Osman Hadzikic (Slaven Belupo)

MABEKI: Sead Kolasinac (Atalanta), Amar Dedic (Benfica), Nihad Mujakic (Gaziantep), Nikola Katic (Schalke 04), Tarik Muharemovic (Sassuolo), Stjepan Radeljic (Rijeka), Dennis Hadzikadunic (Sampdoria), Nidal Celik (Lens)

VIUNGO: Amir Hadziahmetovic (Hull City), Ivan Sunjic (Pafos), Ivan Basic (Astana), Dzenis Burnic (Karlsruher SC), Ermin Mahmic (Slovan Liberec), Benjamin Tahirovic (Brondby), Amar Memic (Viktoria Plzen), Armin Gigovic (Young Boys), Kerim Alajbegovic (RB Salzburg), Esmir Bajraktarevic (PSV Eindhoven)

WASHAMBULIAJI: Ermedin Demirovic (VfB Stuttgart), Jovo Lukic (Universitatea Cluj), Samed Bazdar (Jagiellonia Bialystok), Haris Tabakovic (Borussia Moenchengladbach), Edin Dzeko (Schalke 04)

BRAZIL

MAKIPA: Alisson Becker (Liverpool), Ederson (Fenerbahce), Bento (Al Nassr), Hugo Souza (Corinthians), John Victor (Nottingham Forest), Carlos Miguel (Palmeiras)

MABEKI: Marquinhos (PSG), Thiago Silva (Porto), Gabriel Magalhaes (Arsenal), Gleison Bremer (Juventus), Leo Pereira (Flamengo), Roger Ibanez (Al Ahli), Alexsandro (Lille), Fabricio Bruno (Cruzeiro), Lucas Beraldo (PSG), Vitor Reis (Girona), Murillo (Nottingham Forest), Wesley Franca (Roma), Danilo (Flamengo), Paulo Henrique (Vasco), Vitinho (Botafogo), Alex Sandro (Flamengo), Douglas Santos (Zenit), Luciano Juba (Bahia), Caio Henrique (Monaco), Kaiki Bruno (Cruzeiro), Carlos Augusto (Inter Milan)

VIUNGO: Casemiro (Manchester United), Bruno Guimaraes (Newcastle United), Fabinho (Al Ittihad), Andrey Santos (Chelsea), Danilo (Botafogo), Lucas Paqueta (Flamengo), Gabriel Sara (Galatasaray), Joao Gomes (Wolves), Andreas Pereira (Palmeiras), Joelinton (Newcastle United), Gerson (Cruzeiro), Matheus Pereira (Cruzeiro)

WASHAMBULIAJI: Vinicius Jr (Real Madrid), Raphinha (Barcelona), Matheus Cunha (Manchester United), Luiz Henrique (Zenit), Gabriel Martinelli (Arsenal), Joao Pedro (Chelsea), Neymar (Santos), Endrick (Lyon), Rayan (Bournemouth), Antony (Real Betis), Igor Thiago (Brentford), Pedro (Flamengo), Richarlison (Tottenham), Igor Jesus (Nottingham Forest), Kaio Jorge (Cruzeiro)

SWEDEN

MAKIPA: Viktor Johansson (Stoke City), Kristoffer Nordfeldt (AIK), Jacob Widell Zetterstrom (Derby County)

MABEKI: Hjalmar Ekdal (Burnley), Gabriel Gudmundsson (Leeds United), Isak Hien (Atalanta), Emil Holm (Juventus), Gustaf Lagerbielke (Braga), Victor Lindelof (Aston Villa), Erik Smith (St. Pauli), Carl Starfelt (Celta Vigo), Elliot Stroud (Mjallby), Daniel Svensson (Borussia Dortmund)

VIUNGO: Taha Ali (Malmo), Yasin Ayari (Brighton), Lucas Bergvall (Tottenham), Jesper Karlstrom (Udinese), Ken Sema (Pafos), Mattias Svanberg (Wolfsburg), Besfort Zeneli (Union St-Gilloise)

WASHAMBULIAJI: Alexander Bernhardsson (Holstein Kiel), Anthony Elanga (Newcastle United), Viktor Gyokeres (Arsenal), Alexander Isak (Liverpool), Gustaf Nilsson (Club Brugge), Benjamin Nygren (Celtic)

KIUNGO AFICHUA KINACHOMBEBA ABUYA KOCHA GAMERA AJITOA FUFUNI, NEW CITY YASISITIZA KUTOSHUKA DARAJA