Habari za michezo

MUDATHIR AWASHTUKIA MASHABIKI KISA MWAMNYETO

Vardo May 17, 2026 3:05 pm

KIUNGO wa Yanga SC, Mudathiri Yahya, amezungumza kwa hisia kali akiwakosoa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kile alichodai kuwa wamechangia kumuumiza kisaikolojia nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto.

Mudathiri amesema baadhi ya mashabiki hao wamekuwa wakimtumia Mwamnyeto ujumbe wa kumkatisha tamaa kufuatia tukio la kujifunga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Liti, Singida, Mwamnyeto alijifunga wakati akijaribu kuokoa hatari langoni, hali iliyochangia Yanga kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wameelekeza lawama kwa nahodha huyo, jambo ambalo Mudathiri amesema limeongeza presha na maumivu ya kisaikolojia kwa mchezaji huyo.

Akizungumzia hali hiyo, Mudathiri amesema anamuombea msamaha Mwamnyeto kutokana na presha aliyokutana nayo, akisisitiza kuwa wachezaji wanahitaji kuungwa mkono zaidi kuliko kukosolewa kwa maneno makali wanapokosea uwanjani.

Mudathiri amewataka mashabiki wa Yanga kusimama pamoja na kikosi chao katika kila hali, akisema mafanikio ya timu hayawezi kupatikana bila umoja, uvumilivu na hamasa ya pamoja badala ya lawama za moja kwa moja.

BARKER SIMBA SASA NI FULL MOTO UWANJANI MAEMA NA MUSTAKABALI WAKE SIMBA, VITA YA SAINI YAZIDI KUPAMBA MOTO