Habari za michezo

MANGUNGU AWEKA WAZI SIRI YA MABADILIKO SIMBA

Vardo May 17, 2026 9:44 am

MWENYEKITI wa klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo unaendelea kwa utaratibu maalum huku ukizingatia sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa na mamlaka husika nchini.

Mangungu amesema Simba SC ina mfumo wa kipekee wa uendeshaji unaohusisha pande mbili ambazo ni wanachama pamoja na wawekezaji, hali inayohitaji umakini mkubwa katika kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu maendeleo ya klabu hiyo.

Ameeleza kuwa kutokana na muundo huo, kila hatua inayochukuliwa inalazimika kufuata taratibu rasmi za kisheria ili kuhakikisha mabadiliko yanayofanyika yanakuwa na manufaa kwa klabu pamoja na wadau wake wote kwa ujumla.

“Klabu inaendeshwa kwa pande mbili, wanachama na wawekezaji. Utaratibu unaendelea kama ulivyopangwa kwa kufuata sheria na kanuni za nchi,” amesema Mangungu wakati akizungumzia mwenendo wa mchakato huo ndani ya klabu hiyo.

Mangungu amesisitiza kuwa hakuna jambo lolote la taharuki ndani ya Simba SC, akibainisha kuwa kila kitu kinafanyika kwa utulivu na kwa kufuata mwongozo uliowekwa tangu mwanzo wa mabadiliko hayo kuanza kujadiliwa.

Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho mashabiki wa Simba SC wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa maboresho ya kiuongozi na kiutendaji ndani ya klabu hiyo, huku wengi wakitarajia kuona hatua mpya zitakazoendelea kuijenga timu hiyo kuelekea mafanikio makubwa zaidi ndani na nje ya nchi.

PRESHA YAZIDI KWA MWAMNYETO, AOMBA KUPUMZISHWA YANGA YAWEKA WAZI, HATUOGOPI AZAM WALA MASHUJAA KUCHUKUA UBINGWA