MHHH HAYA YA MSUVA HUKO IRAQ 🫣🫣🫣….AU NDIO MWISHO WA ENZI..?
WAKATI msimu wa Ligi Kuu Iraq ukikaribia mwishoni, mashabiki wa soka Tanzania wanasubiri kushuhudia Simon Msuva akiivunja rekodi yake binafsi ya mabao akiwa na Al Talaba.
Msuva alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu wa 2024/25 akitokea Al Najma ya ligi daraja lwa kwanza Saudia.
Katika msimu wake wa kwanza Al Talaba, winga huyo wa zamani wa Wydad AC alianza kwa kasi kubwa baada ya kufunga mabao 12 kwenye mechi 11, rekodi iliyomfanya kuwa mmoja wa mastaa waliotikisa ligi hiyo kwa kipindi kifupi.
Msimu huu pamoja na ushindani mkubwa, Msuva ameendelea kuonyesha makali yake na katika mechi 25 alizoichezea Al Talaba hadi sasa amefunga mabao manane na kutoa asisti mbili, akihusika kwenye mabao 10.
Takwimu hizo zinaonyesha bado ni mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi hicho kinachoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 35, kikishinda 18, sare nane na kupoteza tisa.
Zikiwa zimesalia mechi tano kumalizaka msimu, ili aivunje rekodi yake ya msimu uliopita ya mabao 12, Msuva anapaswa kufunga mabao matano.
Hesabu zinaonyesha ili avunje rekodi hiyo atalazimika kufunga wastani wa bao moja kwa kila mechi, jambo ambalo linawezekana kutokana na uzoefu wake na uwezo wake mkubwa wa kucheza kwenye maeneo ya mwisho ya ushambuliaji.