NZENGELI AFICHUAA SIRI YA MBIO ZA MABAO, FEI TOTO AWAACHA WENGINE MBALI
USHINDANI wa mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu unaendelea kuchukua sura mpya, huku kiungo wa Yanga SC, Yanga SC, Max Nzengeli akitoa mtazamo wake kuhusu kinachoweza kutokea mwisho wa msimu.
Nzengeli amesema anaamini nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ana nafasi kubwa zaidi ya kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora kutokana na ubora wake unaoendelea kuonekana kila mchezo.
Kwa sasa, Fei Toto anaongoza chati ya mabao akiwa ametupia nyavuni mara 12, akifuatiwa kwa karibu na kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Yanga SC, Allan Okello, pamoja na mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube, ambao wote wakiwa na mabao tisa kila mmoja.
Akizungumzia tofauti hiyo ya mabao, Nzengeli amesema inampa Fei Toto faida kubwa, hasa kutokana na uwezo wake wa kutumia vyema nafasi chache anazopata mbele ya lango la wapinzani.
Pia amesisitiza kuwa ushindani uliopo msimu huu ni mkali kuliko kawaida, jambo linalowafanya washambuliaji na viungo washambuliaji kuongeza juhudi kila mchezo ili kusaidia timu zao pamoja na kuboresha takwimu zao binafsi.
Hata hivyo, Nzengeli hakusita kumzungumzia pia Allan Okello, akimuelezea kama mchezaji mwenye kipaji kikubwa na anayetoa mchango muhimu ndani ya kikosi cha Yanga msimu huu.
“Fei Toto ana nafasi kubwa ya kubeba tuzo kwa sababu anaongoza kwa sasa, lakini pia Okello ni mchezaji mzuri sana na namkubali,” amesema Nzengeli.