Mechi ya Leo Ligi Kuu

SINGIDA YAICHELEWESHA KMC KUSHUKA IKIICHAPA MBEYA CITY

Vardo May 26, 2026 10:24 pm

SINGIDA Black Stars imefanikiwa kulinda heshima yake nyumbani, ikitoa kipigo kikali cha mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Mei 25, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel mkoani Singida.

Ushindi huo unaifanya KMC kushusha pumzi ikisubiri hatma yake katika mechi tano zilizobaki ambapo kama Mbeya City leo ingeshinda, basi ilikuwa inaikatia tiketi KMC kushuka daraja moja kwa moja kufuatia sasa kuwa na pointi tisa, huku Mbeya City ikiwa nazo 22.

Singida imelazimika kutoka nyuma kutengeneza ushindi huo, baada wageni kutangulia kuandika bao mapema dakika ya nne kufuatia Morrice Chukwu kujifunga wakati akipambana kuokoa krosi ya Eliud Ambokile.

Baada ya bao hilo, Singida ikatulia na kufanikiwa kusawazisha na kuongeza lingine kwa mabao mawili yaliyopatikana ndani ya dakika mbili, akitangulia beki Ande Koffi kuirudisha mchezoni timu hiyo kwa shuti kali la mbali likimshinda kipa Sudi Dondola.

Horso Muaku akaandika bao la pili dakika ya 18 akifunga kirahisi wakati akitengenezewa pasi ya mwisho na kiungo Emmanuel Keyekeh, na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko wenyeji wakiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili, Singida ikaendelea kutengeneza ushindi wake ambapo Khalid Aucho aliyeingia kipindi hicho mwanzoni akaandika bao la tatu kwa mkwaju wa penalti dakika ya 83, iliyotokana na Linda Mtange kuchezewa vibaya na Dondola.

Msumari wa nne ukapigiliwa na Mosi Ndumumwe akifunga bao zuri akimalizia krosi ya Mishamo Daudi, mshambuliaji huyo akiandika bao lake la tisa msimu huu akiongoza kwa ufungaji ndani ya kikosi hicho, huku akimfikia Prince Dube wa Yanga, pia akiwa nyuma ya kinara Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam mwenye 14 na Allan Okello wa Yanga akifunga 11.

Matokeo hayo yanaifanya Singida kurejea nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 41, ikiishusha JKT Tanzania iliyokuwa hapo na pointi zake 38.

MWAJANGA AIPA PRISONS POINTI TATU, PAMBA JIJI IKILOA KILUMBA Thể thao 79win mang đến trải nghiệm giải trí sôi động cho người yêu thích cá cược trực tuyến