Habari za michezo

DODOMA JIJI IMEWASHIKIA HAPA VIGOGO

Vardo May 27, 2026 10:23 am

KOCHA wa Dodoma Jiji, Aman Josiah amesema anapokutana na klabu zenye viwango vya juu kama Simba na Yanga, benchi la ufundi linakuwa limefanya uchambuzi wa kina kujua ubora na udhaifu wa wapinzani wao.

Amesema Simba na Yanga mara nyingi hazibadilishi sana vikosi vyao na mipango inakuwa ni kushambuliaji na kumiliki mpira, hivyo wapinzani kama wanakuwa hawajajipanga kuzizuia mbinu zao inakuwa ni ngumu kuwakabili.

“Klabu hizo plani zao kubwa inakuwa ni kushambuliaji, kama benchi la ufundi tunatafuta mbinu jinsi ya kuzipa chalenji kwa kuwapa majibu wachezaji ya kipi wakifanye wakiwa uwanjani, pia inakuwa ni nafasi kwao kuonyesha ubora wao,” amesema kocha huyo.

“Ndiyo maana unaweza ukaona matokeo baada ya kukutana na timu hizo kwa nyakati tofauti, tunachokizingatia ni kuwa miongoni mwa timu zenye ushindani wa juu.”

Dodoma Jiji chini ya kocha huyo msimu huu, ilifungwa na Yanga mabao 3-1 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Januari 27, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar, kisha mzunguko wa pili Mei 13, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel mkoani Singida, ilishinda 3-2.

Kwa upande wa Simba, imekutana na Dodoma Jiji mara tatu msimu huu, moja ikiwa mechi ya Kombe la Shirikisho la CRDB hatua ya 16 bora ambapo Wekundu wa Msimbazi walishinda kwa mabao 3-1, Aprili 12, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Katika ligi, mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Februari 25, 2026 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, timu hizo zilishindwa kufungana, lakini mzunguko wa pili Mei 24, 2026 kwenye Uwanja wa  KMC Complex, Dar, Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Matokeo hayo ambayo Dodoma Jiji imejaribu kuonyesha ushindani kwa Simba, imemfanya Josiah kusema: “Kadri unavyocheza na klabu hizo unakuwa unagundua ni mbinu gani utumie ili kuhakikisha tunafanikiwa plani zetu.”

Thể thao 79win mang đến trải nghiệm giải trí sôi động cho người yêu thích cá cược trực tuyến WALIOCHEZA KOMBE LA DUNIA NA UMRI MDOGO