Azam FC

AZAM YAMWITA MEZANI HIMID MAO

Vardo May 29, 2026 9:30 am

MATAJIRI wa Chamazi, Azam FC wameanza mazungumzo na kiungo wao mkabaji Himid Mao kwa lengo la kuongezea mkataba baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba wanyatia huduma yake.

Ingawa tetesi za Simba hazina nguvu sana kuliko za Azam ili kumsainisha mkataba mpya itatakiwa kutoa pesa ndefu kuliko aliyopewa wakati anarejea tena klabuni hapo, hiyo ni baada ya nyota huyo kuonyesha kiwango cha juu.

Kwa mara ya kwanza Mao aliichezea Azam kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 kisha akaenda kujiunga na Petrojet(2018/19),ENPPI(2019-2021),Ghazl El Mahalla(2021/22),Tala’ea El-Gaish SC(2022-2025) kabla ya kurejea Azam ambapo alisajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Chanzo hicho kilisema:”Tayari mazungumzo mapya yameanza, ingawa siyo rahisi kwani anahitaji pesa ndefu, lakini bado viongozi wanaendelea kuzungumza naye.

Kiliongeza chanzo hicho:”Viongozi wanazungumza na wachezaji mbalimbali waliyomaliza mikataba yao kwa kumhusisha kocha Florent Ibengé ambaye tunaamini ndiye eneo lake sahihi la kutoa mapendekezo na ripoti yake ndiyo itakayotumika kusajili wengine wapya.”

Staa wa zamani wa Azam,Erasto Nyoni anayeichezea Kagera Sugar ya Championship, amesema:”Kiwango cha mchezaji ndiyo thamani ya pesa yake katika usajili, wakati Himid anarejea Tanzania na kujiunga Azam wengi waliona timu hiyo kama inakosa malengo sasa amewaonyesha kwa vitendo.”

AMANI JOSIAH, MINZIRO KAZI ZINAZUNGUMZA WENGER ASEMA SERENGETI BOYS NI MUSTAKABALI MPYA WA SOKA AFRIKA