Yanga SC

MBINGWA YANGA WAANZA MAPEMA USAJILI MKUBWA WA MSIMU UJAO

Vardo May 31, 2026 12:26 pm

Yanga SC wameanza kwa kasi kuweka msingi wa kikosi chao kuelekea msimu ujao, baada ya kufungua mazungumzo ya awali yanayomhusisha kiungo mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Adama Coulibali, katika mpango unaoashiria dhamira ya kuongeza nguvu kikosini.

Kwa mujibu wa taarifa za karibu na masuala ya usajili, uongozi wa Yanga umeanza mawasiliano ya moja kwa moja na upande wa menejimenti ya mchezaji huyo, lengo likiwa ni kufahamu hali yake ya usajili pamoja na uwezekano wa kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania.

Ingawa mazungumzo hayo bado yapo katika hatua za awali, pande zote mbili zinaendelea kupima masharti na mazingira ya mkataba huo, huku kila upande ukitathmini uwezekano wa kufikia makubaliano kabla ya dirisha rasmi la usajili kufunguliwa.

Yanga wanadaiwa kuwa na mpango wa kumaliza mazungumzo hayo mapema, ili endapo makubaliano yatapatikana, mchezaji huyo aweze kujiunga mapema na maandalizi ya pre-season pamoja na kikosi chake kipya.

Coulibali anaweza kuwa miongoni mwa usajili mkubwa zaidi wa Yanga kuelekea msimu ujao, kutokana na uzoefu wake mkubwa katika soka la Afrika akiwa na Al Hilal.

Kiungo huyo anatambulika kwa uwezo wake wa kutengeneza nafasi na mchango wake katika michezo mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo linalomfanya kuonekana kama nyongeza muhimu kwa kikosi cha Yanga.

Uongozi wa Yanga unaendelea na mkakati mpana wa kusajili wachezaji wenye ubora na uzoefu wa kimataifa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuongeza ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao.

SIMBA SC YAANZA OPERESHENI ALAMA 15, YAREJEA KAMBINI KWA VITA YA UBINGWA MPANGO WA SIRI WA SIMBA WAMHUSISHA BEKI WA MAMELODI SUNDOWNS