Yanga SC

OKELLO NDANI YA ORODHA YA WAFUNGA HAT TRICK LIGI KUU

Vardo June 28, 2026 10:16 am

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Allan Okello, amejiunga rasmi kwenye orodha ya wachezaji waliofunga hat-trick katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26, katika mchezo dhidi ya TRA United.

Katika mcheso huo Yanga ameibuka na ushindi wa manao 3_0 dhidi ya TRA United mchezo uliochezwa uwanja wa KMC Complex, Mwenge.

Mabao yote yamefungwa na OkEllo na anakuwa mchezaji wa nne kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja msimu huu, akifuata nyayo za Mossi Nduwumwe wa Burundi, Mathew Tegisi wa Kenya na Fabrice Ngoy wa DR Congo.

Nduwumwe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika rekodi hiyo baada ya kufunga hat-trick dhidi ya Dodoma Jiji, huku Tegisi akifanya hivyo alipokutana na Mtibwa Sugar.

Kwa upande wake, Ngoy aliingia kwenye orodha hiyo baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya KMC, kabla ya Okello kukamilisha idadi ya wafungaji hao kwa hat-trick yake dhidi ya TRA United.

Hat-trick ya Okello imezidi kuthibitisha ubora wake msimu huu, ambapo amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na mchango wake mkubwa wa mabao na pasi za mwisho.

Rekodi hiyo pia inaonyesha ushindani mkubwa uliokuwepo katika Ligi huyo kwa 2025/26, huku wachezaji kutoka mataifa tofauti wakionyesha uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na kuandika historia zao ndani ya ligi hiyo.

YANGA WATANGAZA OKELLO DAY YA KIBABE DHIDI YA JKT MBOGO, MKONGWE YANGA ANAYESIMAMA NA PACOME, CHAMA