YANGA WATANGAZA OKELLO DAY YA KIBABE DHIDI YA JKT
MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, ametoa wito kwa mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Juni 30, 2026, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, akitangaza siku hiyo kuwa “Okello Day.”
Kamwe ametoa kauli hiyo mara baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United, akieleza kuwa mchezo unaofuata utakuwa wa kipekee na umetengwa kwa ajili ya kumuunga mkono nyota wa timu, Okello.
Amesema anaamini Yanga itaendelea na mwendo wake mzuri licha ya kutarajia upinzani mkali kutoka kwa JKT Tanzania, huku akisisitiza kuwa sapoti ya mashabiki itakuwa silaha muhimu katika kuhakikisha timu inapata ushindi.
“Kuna sehemu inakwenda, aibu wataona wao. Natangaza rasmi kuwa mechi ya Jumanne dhidi ya JKT Tanzania ni Okello Day. Najua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaamini tutafanya vizuri,” amesema Kamwe.
Mashabiki wa Yanga, ambao sasa wanasubiri kwa hamu kushuhudia kile kitakachotokea kwenye Okello Day, huku wengi wakiamini nyota huyo ataendelea kuonyesha kiwango bora na kuiongoza timu yake kupata matokeo chanya