Mnigeria Mambo Magumu Azam
UONGOZI wa Azam FC huenda ukaachana na winga wa kikosi hicho Mnigeria, Abel Abah baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tangu alipojiunga rasmi na matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Januari 30, 2026, akitokea Klabu ya KF Tirana ya Albania.
Kipre aliyeondoka Azam FC msimu 2023-2024, akiwa ameifungia timu hiyo mabao tisa ya Ligi Kuu na kujiunga na MC Algiers ya Algeria, amerejea tena ndani ya kikosi hicho jambo linaloweka nafasi ya Mnigeria huyo shakani kwa msimu wa 2026-2027.
Abah alijiunga na Azam FC mwishoni mwa dirisha dogo la Januari 2026, ili kuongezea nguvu kikosi hicho, akichukua nafasi ya Mtunisia Baraket Hmidi aliyeondoka kwa mkopo na kujiunga na Diyala SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Iraq.
“Suala la mchezaji kuondoka au kubakia itategemea na ripoti ya benchi la ufundi ila ni kweli wapo wengine tutakaoachana nao kama ilivyo utaratibu wa kila msimu unapoisha, kwa sasa tusubirie uamuzi wa mwisho kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumza na Soka La Bongo, Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Azam, Rashid Seif alisema kinachoendelea kwa sasa ni tetesi tu kama ilivyokuwa kawaida ya kila dirisha la usajili linapofunguliwa, ingawa taarifa rasmi zitatolewa na klabu hiyo.