Burudani

Dulla Makabila Achanganyikiwa: “Najuta Kumpa Talaka Zaiylissa, Natafuta Mwanasaikolojia”

Vardo July 17, 2026 2:05 pm

Inasikitisha! Dulla Makabila Achanganyikiwa Baada ya Kumpa Talaka Zaiylissa, Sasa Anatafuta Mwanasaikolojia

Staa wa muziki wa Singeli nchini, Dulla Makabila, amefunguka mazito moyoni mwake na kukiri kuwa bado anateseka kiakili tangu alipoamua kuachana na aliyekuwa mke wake, Zaiylissa. Msanii huyo amebainisha kuwa kwa sasa yuko kwenye mpango wa kutafuta msaada wa mwanasaikolojia ili aweze kumsahau kabisa mzuri huyo.

Akizungumza na Soka la Bongo, Dulla Makabila ameweka wazi kuwa uamuzi wa kumpa talaka Zaiylissa ulikuwa wa hasira na hadi leo hii unamtesa, huku akijikuta akijilaumu kila anapokuwa peke yake.

“Natafuta mwanasaikolojia anisaidie nimsahau. Kila nikikaa peke yangu namkumbuka sana, na hata nikikutana naye sehemu yoyote nachanganyikiwa. Kuna wakati najutia kabisa kwa nini nilimpa talaka,” alifunguka Dulla Makabila kwa majonzi.

Hasira Zaponza Ndoa ya Miezi Mitatu!

Hii si mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kuonyesha kuwa bado “amenaswa” kwenye dhoruba ya penzi la Zaiylissa. Huko nyuma, Dulla amewahi kukiri hadharani kwamba anajuta kutoa talaka hiyo akiwa na hasira, na bado anahisi maumivu makali kila anapoona picha au taarifa zinazomuhusu mwanamke huyo akiendelea na maisha yake mapya.

Kumbuka kuwa wawili hao walifunga ndoa ya kifahari mwezi Mei 2023, lakini kwa masikitiko makubwa ndoa hiyo ilidumu kwa takribani miezi mitatu tu kabla ya kuvunjika rasmi.

Hadi sasa, sakata la wawili hawa limeendelea kuwa gumzo kubwa kwenye tasnia ya burudani nchini Tanzania, huku mashabiki wengi wakijiuliza kama kuna nafasi ya wawili hawa kurudiana au ndio basi tena!

Siri Ya Kimya Cha Linah Sanga: Ndege Mnana Aliyesusa Bongofleva? Jonathan Sowah Aaga Simba SC Kwa Hisia; Arejea Rasmi Timu Hii!