Simba SC

Jonathan Sowah Aaga Simba SC Kwa Hisia; Arejea Rasmi Timu Hii!

Vardo July 17, 2026 2:15 pm

BAADA ya kurejea katika klabu yake ya zamani ya Singida Black Stars, aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Jonathan Sowah, ameaga rasmi Wekundu wa Msimbazi kwa ujumbe wa hisia uliojaa shukrani na heshima.

Sowah amekamilisha kurejea Singida Black Stars kuelekea msimu wa 2026/27, akifungua ukurasa mpya wa maisha yake ya soka baada ya kuitumikia Simba kwa kipindi kilichokuwa na changamoto na mafunzo mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, mshambuliaji huyo amesema muda aliokaa Simba ulimjengea uzoefu mkubwa na kumbukumbu ambazo ataendelea kuzithamini katika maisha yake ya soka.

Amesisitiza kuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kuivaa jezi ya moja ya klabu kubwa nchini.

Sowah aliwashukuru viongozi wa Simba, benchi la ufundi, wachezaji wenzake pamoja na wafanyakazi wote wa klabu kwa imani na ushirikiano waliompa akiwa sehemu ya familia ya Wekundu wa Msimbazi.

Pia amewapongezi mashabiki wa Simba kwa sapoti yao ya dhati, akieleza kuwa wao ndio moyo wa klabu kutokana na namna walivyoendelea kuisapoti timu katika nyakati zote.

“Ninaondoka nikiwa na shukrani na heshima tu. Natamani Simba SC ipate mafanikio makubwa zaidi katika kila kitu kinachokuja. Asante sana,” aliandika Sowah katika ujumbe wake wa kuaga.

Sasa mshambuliaji huyo anaanza safari mpya akiwa Singida Black Stars, klabu aliyowahi kuitumikia kabla ya kuhamia Simba, akiwa na matumaini ya kurejea katika kiwango chake bora msimu ujao.

Dulla Makabila Achanganyikiwa: “Najuta Kumpa Talaka Zaiylissa, Natafuta Mwanasaikolojia” Kocha Mngqithi Ndiye Aliyesuka Kikosi Kipya cha Yanga SC! Ali Kamwe Athibitisha