Usajili wa Mtibwa Sugar
Michezo Bongo

Fredrick Magata Na Mastaa Wa Mtibwa Sugar Wavamia Ligi Kuu

Vardo July 18, 2026 10:31 am

Licha ya Mtibwa Sugar kushuka daraja msimu wa 2025-2026, wachezaji wa kikosi hicho wamegeuka lulu sokoni. Klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara zinapigana vikumbo kuwania saini zao kutokana na viwango bora walivyoonyesha msimu uliopita.

Katika msimu wa 2025-2026, wakata miwa hao wa Turiani walishuka daraja kwenda Ligi ya Championship baada ya kumaliza nafasi ya 15 wakiwa na alama 27. Mtibwa ilishinda mechi 6, sare 9, na kupoteza michezo 15 kati ya 30, huku ikiungana na KMC FC iliyoburuza mkia kwa alama 9.

Wakati maumivu ya kushuka daraja yakiendelea, kiungo mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Fredrick Magata, amekamilisha dili la kujiunga na maafande wa JKT Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili. Magata ndiye aliyekuwa kinara wa mabao Mtibwa Sugar msimu uliopita, akifunga mabao matano na kutoa pasi za mabao (asisti) mbili, akihusika kwenye mabao 7 kati ya 25 yaliyofungwa na timu nzima.

Hii si mara ya kwanza kwa nyota huyu kung’ara. Msimu wa 2024-2025, Magata alihusika kwenye mabao 30 kati ya 58 ya Mtibwa (akifunga 9 na kuasisti 21), na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Championship kwa alama 71 na kupanda Ligi Kuu wakiambatana na Mbeya City. Rekodi zinaonyesha Magata ni mtaalamu wa kupandisha timu, kwani alifanya hivyo na Mbeya Kwanza (2021-2022) kabla ya kurudia maajabu hayo na Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Soka La Bongo, Magata amekiri kuwepo kwa mazungumzo na klabu mbalimbali lakini akasita kutaja timu mpya kwa madai kuwa mambo hayajakuwa rasmi. Hata hivyo, taarifa za ndani zinathibitisha kuwa tayari amesaini JKT Tanzania, ambapo ataungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Mtibwa, golikipa Constantine Malimi na kiungo mshambuliaji Ismail Mhesa.

Mbali na hao, mastaa wengine waliohama Mtibwa ni aliyekuwa beki wa kati na nahodha, Haroun Lyawatwa aliyetua Mashujaa FC, pamoja na beki wa kulia Datius Peter aliyetimkia Geita Gold.

Burudani Ya Sloti Inapatikana Ukicheza Rumble Kong CASHINGO Hispania Vs Argentina Kukutana Vitani Atlanta!