Michezo Bongo

Ratiba NBC 2026/2027: Simba Vs Yanga Kukipiga Oktoba 10 Uwanja Wa Uhuru

Vardo July 20, 2026 12:45 pm

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) leo Jumatatu, Julai 20, 2026, imetoa rasmi ratiba mpya ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2026/2027. Katika ratiba hiyo, mchezo wa kwanza wa Watani wa Jadi, Simba SC na Yanga SC, unatarajiwa kupigwa Oktoba 10, 2026.

Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza utashuhudia Simba wakiwa wenyeji katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ukianza majira ya saa 1:00 usiku. Hatua hii inafanya timu hizi kongwe nchini kukutana mara sita (6) ndani ya mwaka huu wa 2026 tu.

Safari ya Kariakoo Derby Mwaka 2026:

  • Mechi 2 za Ligi Kuu msimu uliopita

  • Mechi 1 ya Kombe la Muungano

  • Ngao ya Jamii (Agosti 12, 2026)

  • Mzunguko wa 1 Ligi Kuu (Oktoba 10, 2026)

  • Mzunguko wa 2 Ligi Kuu (Februari 6, 2027 – Yanga akiwa Mwenyeji Uhuru)

Ligi Kuu Kuanza Agosti 14 Msimu mpya wa NBC Premier League utaanza rasmi Agosti 14, 2026, kwa michezo mitatu ya ufunguzi:

  1. Pamba Jiji vs Dodoma Jiji: Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza (Saa 8:00 mchana).

  2. Mbeya City vs Geita Gold: Uwanja wa Sokoine, Mbeya (Saa 10:15 jioni).

  3. Singida Black Stars vs Fountain Gate: Uwanja wa Airtel, Singida (Saa 1:00 usiku).

Mbali na kuanza kwa ligi, kurejea kwa Uwanja wa Uhuru baada ya maboresho ya muda mrefu ni habari njema kwa mashabiki, huku Simba na Yanga zikiutumia kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu huu.

Kelvin Nashon Afunguka Mwanzo Wake Simba SC: “Nimepokelewa Vizuri Ratiba Ya Kariakoo Derby 2026/27: Simba Vs Yanga Kukutana Mara 3