Kelvin Nashon Simba SC
Simba SC

Kelvin Nashon Afunguka Mwanzo Wake Simba SC: “Nimepokelewa Vizuri

Vardo July 20, 2026 12:39 pm

Kiungo mpya wa Simba SC, Kelvin Nashon, ameanza maisha yake mapya ndani ya kikosi hicho kwa tabasamu na ari kubwa, huku akibainisha kuwa mapokezi mazuri kutoka kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi yamemsaidia kuondoa presha ya kujiunga na klabu hiyo kubwa.

Nashon, aliyejiunga na Wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu wa 2026/27, ameeleza kuwa kwa sasa nguvu na akili zote zimeelekezwa kwenye maandalizi ya msimu ili kuhakikisha kila mchezaji anakuwa katika kiwango bora cha kuipigania timu.

Akizungumzia hali ya kambi, kiungo huyo mkabaji amekiri kuwa kuna ushindani mkubwa wa namba, lakini ni ushindani wenye afya unaomfanya kila mchezaji kuwajibika kikamilifu.

“Nimefurahi sana kujiunga na Simba, na wala sijajihisi mgeni kwa sababu wamenipokea vizuri mno. Mbele yetu kuna mashindano magumu, hivyo kila mmoja yupo makini mazoezini. Ukipoteza umakini kidogo tu, unaweza kupoteza nafasi yako,” amesema Nashon.

Aidha, Nashon amebainisha kuwa mazingira ya Msimbazi yanatofautiana na klabu yake ya zamani kutokana na kiu kubwa ya mafanikio iliyopo klabuni hapo, jambo linalomfanya kila mchezaji kupambana bila kukata tamaa.

Kwa sasa Simba SC inaendelea na maandalizi makali ya msimu mpya ikilenga kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.

Simba SC Yaanza Kambi Msimu Mpya: Matola Afunguka Hali Ya Wachezaji Na Usajili Mpya Ratiba NBC 2026/2027: Simba Vs Yanga Kukipiga Oktoba 10 Uwanja Wa Uhuru