Singida Black Stars vs Mogadishu City
Singida Big Stars FC

Singida BS Waichapa Mogadishu 4-1 CECAFA Kagame, Wawawasha Simba SC!

Vardo July 29, 2026 9:29 am

KIGALI, RWANDA: Bingwa mtetezi wa Kombe la CECAFA Kagame, Singida Black Stars, imerejesha matumaini makubwa ya kutetea taji hilo baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Mogadishu City katika mchezo wa Kundi B uliopigwa kwenye Uwanja wa Pele, Kigali nchini Rwanda.

Baada ya kuanza vibaya michuano hiyo kwa kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Jamus SC katika mchezo wa kwanza, Singida Black Stars iliingia uwanjani ikiwa na shauku kubwa ya ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Mchezo Ulivyokuwa

Mogadishu City ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya 10 kupitia kwa Naby Bangoura, aliyetumia vyema nafasi aliyoipata na kuwapa Wasomalia hao matumaini ya ushindi wa kwanza, kufuatia suluhu yao ya awali dhidi ya Simba SC.

Hata hivyo, Singida Black Stars haikukata tamaa. Dakika tatu tu baadaye (dakika ya 13), kiungo mpya Henry David aliisawazishia timu yake kabla ya Mathew Tegisi kuongeza bao la pili dakika ya 16 na kubadilisha kabisa upepo wa mchezo.

Kabla ya kwenda mapumziko, Henry alirejea tena kambani dakika ya 44 na kufunga bao lake la pili, na kuifanya Singida kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa kutoka kwa Singida BS, na mnamo dakika ya 53, Tegisi naye alihitimisha ushindi kwa kufunga bao la nne la timu hiyo na la pili kwake binafsi.

Nguvu ya Usajili Mpya

Ushindi huu umethibitisha ubora na thamani ya ingizo jipya ndani ya kikosi cha Singida Black Stars, kwani mabao yote manne yalifungwa na wachezaji wapya:

  • Henry David (aliyetokea Fountain Gate) – Mabao 2

  • Mathew Tegisi (aliyetokea Pamba Jiji) – Mabao 2

Kazi Ipogo Dhidi ya Simba SC!

Matokeo haya yanaifanya Singida BS kufufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali, ambapo sasa inasubiri mchezo wake wa mwisho wa kundi dhidi ya Simba SC—mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo wakiwa wametwaa ubingwa mara sita. Mchezo huo ndio utakaotoa hatima ya timu hizo katika Kundi B.

KVZ SC vs Al Hilal SC: Mtihani Mzito CECAFA Kagame Cup LEO Barker Athibitisha Ujio wa Neo Maema Simba SC Msimu Mpya