Hatima ya Depu Yanga
Yanga SC

Ukweli WKuhusu Hatima ya Depu Yanga Na Petro de Luanda

Vardo August 6, 2026 11:00 am

HATMA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurelio ‘Depu’, imeendelea kuwa gumzo kubwa ndani ya kikosi cha Yanga SC baada ya mabingwa hao wa Soka Tanzania Bara kuthibitisha kupokea ofa kibao za kumuwania nyota huyo kutoka ndani na nje ya nchi.

Ingawa mshambuliaji huyo bado ana mkataba na Yanga, uongozi wa Wananchi umeweka wazi kuwa mustakabali wake kwa msimu mpya bado haujakamilika, huku maamuzi ya mwisho yakitegemea ushauri na tathmini ya benchi la ufundi.

Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, ameeleza kuwa klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya kina na kocha mkuu ili kubaini kama Depu bado yupo kwenye mipango ya kiufundi ya msimu ujao au kama watamuuza.

“Depu ana ofa nyingi mezani. Hivi sasa tunashauriana na benchi la ufundi kuona kama kocha bado anamhitaji. Kama yumo kwenye mipango tutabaki naye, lakini kama sivyo, tutafungua milango ya kufanya biashara,” alisema Kamwe.

Petro de Luanda Yataka Saini ya Depu

Katika hatua nyingine, Kamwe amethibitisha kuwa miamba ya soka nchini Angola, Petro de Luanda, imewasilisha ofa rasmi mezani kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo. Hata hivyo, amesisitiza kuwa pande hizo mbili bado hazijafikia makubaliano ya mwisho.

“Ni kweli tumepokea ofa rasmi kutoka Petro de Luanda wakimtaka Depu, lakini hadi sasa mazungumzo yanaendelea na hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa,” aliongeza.

Depu alitua Yanga akiwa na matarajio makubwa kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao na uzoefu wake kwenye mashindano ya kimataifa. Klabu hiyo sasa ipo kwenye mchakato wa kusuka kikosi cha ushindani zaidi, na maamuzi ya mwisho kuhusu nyota huyo yatizingatia maslahi ya kiufundi na ya kifedha ya klabu.

Ukweli wa Fei Toto Kutakiwa Simba na Yanga Huu Hapa! Kocha Barker Afichua Mpango Mzito Simba SC Baada ya Kurejea Rwanda