Manqoba Mngqithi Yanga
Yanga SC

Mngqithi Afunguka Kipigo Kizito cha Yanga Siku ya Mwananchi

Vardo August 10, 2026 9:31 am

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, ameweka wazi hisia zake bila kuficha chochote, akibainisha kuwa uzembe na makosa ya kizembe kutoka kwa wachezaji wake ndivyo vilivyoigharimu timu hiyo katika kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Aigles du Congo.

Mabingwa hao watetezi walitamatisha tamasha lao la Siku ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kwa matokeo yasiyoridhisha mbele ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kushangilia kikosi chao kipya.

Licha ya kwamba mchezo huo ulikuwa wa kirafiki kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2026/27, Mngqithi raia wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa viwango vya makosa yaliyofanyika havistahili kushuhudiwa kwenye timu kubwa kama Yanga.

β€œTulifungwa bao la kijinga sana. Tulifanya makosa ya kijinga uwanjani. Lazima niwe mkweli na wazi uwanja mzima uone,” alisema Mngqithi kwa msisitizo baada ya filimbi ya mwisho.

Kauli hii nzito inakuja wakati kocha huyo akiendelea kusuka safu yake na kupandikiza falsafa mpya ya uchezaji. Kwa upande wake, mchezo huu umekuwa jicho la pili la kumsaidia kubaini mapungufu mapema kabla ya mechi rasmi za ushindani kuanza.

Safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana kupoteza umakini kwenye nyakati muhimu, jambo lililowapa Aigles du Congo mianya ya kushambulia na kupata mabao hayo ya ushindi.

Kwa sasa, kibarua kikubwa kilichopo mbele ya Mngqithi na benchi lake la ufundi ni kurekebisha safu hiyo ya ulinzi na kuhakikisha wachezaji wanajifunza kutokana na makosa hayo ili kuingia kwenye msimu mpya wakiwa imara zaidi.

DJ Ally B Avunja Mwiko Yanga Day: Apiga Shoo ya Moto na Kuteka Uwanja wa Uhuru! Simba SC Waelekea Zanzibar Kuikabili Yanga Ngao ya Jamii 2026