Simba Yapatwa na Pigo Zito: Nickson Kibabage Nje Wiki 4!
Kikosi cha Simba SC kimekumbana na pigo zito kuelekea mechi zake za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, baada ya beki wake wa kushoto, Nickson Kibabage, kugundulika kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne kufuatia majeraha ya misuli ya paja (hamstring).
Kibabage alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2026/2027 dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Agosti 16, 2026, katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mtego kwa Steve Barker Eneo la Ulinzi
Kukosekana kwa Kibabage kunaiweka Simba kwenye mtihani mgumu, kwani pia inamkosa Antony Mligo anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars. Mligo anatakiwa kukosa jumla ya mechi tatu za Ligi Kuu.
Kutokana na changamoto hiyo katika eneo la ulinzi wa kushoto, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, anatarajiwa kumtumia beki wa kulia, Nathaniel Chilambo, ambaye ana uwezo wa kumudu vyema nafasi hiyo ya kushoto kama alivyokuwa akifanya alipokuwa Azam FC.
Taarifa ya Daktari na Maendeleo ya Majeraha
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa Kibabage anaendelea vizuri na matibabu na anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya mapumziko hayo ya kijiuguza.
Aidha, Ahmed Ally ametoa updates za wachezaji wengine majeruhi:
-
Mahamadou Tanja Kassali (Kipa): Anaendelea vizuri na matibabu ya dawa (hatafanyiwa upasuaji) baada ya kuumia dhidi ya Kagera Sugar.
-
Yusuph Kagoma: Alipewa mapumziko na madaktari ili kumpa muda wa kupona kikamilifu kabla ya kurejea kikosini.