Simba SC vs Mighty Wanderers
Simba SC

Kocha Simba Awaonya Wachezaji Wake Dhidi ya Mighty Wanderers: “Kazi Bado Haijamalizika”

Vardo September 10, 2026 9:55 am

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ametoa onyo kali kwa wachezaji wake dhidi ya kulewa matokeo ya mchezo wa kwanza na kutoridhika kuelekea pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.

Barker amesisitiza kuwa bado kazi haijakamilika, na uzembe wowote katika mchezo huo wa marudiano utakaopigwa Siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, unaweza kuwagharimu na kuwapa nafasi wapinzani wao kurejea mchezoni.

Kujirekebisha na Kufanyia Kazi Makosa Benchi la ufundi la Simba limefanya tathmini ya kina kuhusu mchezo wa kwanza ili kubaini maeneo yaliyofanya vizuri na yale yanayohitaji marekebisho ya haraka. Barker alieleza kuwa kukutana na mpinzani huyo ndani ya muda mfupi kuwawzesha kuwafahamu vizuri kiutendaji.

“Tunapaswa kufanya tathmini ya mchezo wetu, kuangalia tulifanya vizuri wapi na wapi tunahitaji kuboresha. Hakuna nafasi ya kufanya makosa,” alisema Barker.

Mtazamo Chanya na Presha ya Nyumbani Simba inaingia kwenye mchezo huo ikilenga kupata ushindi mnono mbele ya mashabiki wake wa nyumbani. Hata hivyo, Kocha Barker amewataka wachezaji wake kuonyesha ujasiri, nguvu, na msukumo wa juu kuanzia filimbi ya kwanza hadi ya mwisho.

Ameongeza kuwa kucheza nyumbani ni fursa na jukumu kubwa la kuhakikisha wanapata matokeo chanya ili kusonga mbele katika mashindano haya makubwa ya klabu barani Afrika.

Makgalwa Afichua Sababu ya Kuikataa Yanga na Kujiunga na Simba Yanga vs Gaborone United: Ali Kamwe Afunguka Maandalizi, Majeraha na Big Screen Azam Complex