De Zerbi Tottenham
Michezo Bongo

De Zerbi matatani Tottenham: Mambo yaharibika Spurs baada ya kutumia Bilioni 1.1 Trillion!

Vardo September 11, 2026 6:43 pm

LONDON, ENGLAND – Kocha mkuu wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, ameanza kuingia kwenye shinikizo kubwa kufuatia matokeo mabovu ya timu hiyo mapema msimu huu wa Ligi Kuu England (EPL), licha ya klabu hiyo kumwaga Pauni milioni 332 (zaidi ya Sh bilioni 1,100) kwenye usajili wa wachezaji wapya 10.

Tottenham iliingia kwenye msimu huu ikiwa na matumaini makubwa baada ya kufanya usajili wa kishindo, huku mashabiki wakitarajia kuona kikosi kikirejea kwenye mbio za kuwania nafasi za juu na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Hata hivyo, mambo yamekuwa tofauti kabisa uwanjani. Spurs imeshindwa kuondoka na ushindi katika mechi zake tatu za kwanza za ligi, huku ikiwa haijafunga bao hata moja kufikia sasa.

Mfululizo wa Matokeo Mabaya Timu hiyo ilianza kwa kupoteza dhidi ya Brentford na Newcastle United, kabla ya kuambulia pointi moja pekee baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Nottingham Forest.

Katika mchezo huo dhidi ya Forest, Tottenham ilionyesha kiwango kisichoridhisha baada ya kushindwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango (shot on target)—jambo ambalo halijawahi kuwatokea kwenye mchezo wa ligi kwa zaidi ya miaka minne.

Ushambuliaji na Namba Zinzostua Tatizo la Spurs halipo kwenye ufungaji pekee, bali pia kwenye utengenezaji wa nafasi za wazi. Takwimu zinaonyesta timu hiyo ipo mkiani kwa ubora wa mashuti, huku ikiwa ya tatu kutoka chini kwa uwezekano wa kufunga mabao (Expected Goals – xG).

De Zerbi amekuwa akihangaika kutafuta safu sahihi ya ushambuliaji. Katika mechi zake 10 za hivi karibuni za ligi tangu achukue mikoba ya kuifundisha timu hiyo, ametumia wachezaji 10 tofauti kwenye nafasi tatu za mbele.

Matatizo haya pia yamechangiwa na majeraha ya wachezaji muhimu kama Mohammed Kudus, Dejan Kulusevski, na James Maddison, ambao wamekuwa wakipambana kurejea kwenye utimamu wa mwili.

Kiwango cha Utimamu wa Mwili (Fitness) Mbali na ukame wa mabao, Tottenham pia inaonekana kuzidiwa nguvu na kasi na wapinzani wao. Katika mechi zote tatu za kwanza za ligi, wamerekodiwa kukimbia umbali mdogo kulinganisha na timu walizocheza nazo.

Licha ya mwanzo huu mgumu, uongozi wa klabu bado unaonekana kumpa muda De Zerbi ili kuunganisha kikosi chake kipya. Hata hivyo, matumizi makubwa ya fedha kwenye dirisha la usajili yanamwekea presha ya kuanza kutoa matokeo ya haraka, huku mchezo unaofuata dhidi ya Everton ukionekana kuwa mtihani mwingine mzito kwake.

Wafungaji Bora Wa Muda Wote Ligi Ya Mabingwa Ulaya (Orodha Mpya) Ufaransa U-20 Yaipiga Ecuador 3-2 Kombe la Dunia 2026