CEO wa Simba
Simba SC

CEO Wa Simba Awasha Moto: Atoa Kauli Nzito Dabi ya Kariakoo Na Kimataifa!

Vardo October 4, 2026 9:28 am

Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC, Zubeda Kasuru, amebainisha kuwa ubingwa wa Ngao ya Jamii uliotwaliwa na kikosi cha wanawake, Simba Queens, umeleta hamasa na morali kubwa ndani ya klabu hiyo kuelekea mechi ngumu za mwezi huu wa Oktoba.

Simba Queens walitwaa taji hilo baada ya kuichapa JKT Queens bao 1-0, matokeo ambayo Kasuru anaamini yamejenga hali chanya na kujiamini kwa kikosi cha wakubwa (Senior Team) kinachojiandaa na majukumu mazito ya ligi na kimataifa.

Maandalizi ya Dabi ya Kariakoo

Akizungumzia maendeleo ya timu, CEO Kasuru ameeleza kuwa anaendelea vyema na programu ya klabu akiwa nchini Afrika Kusini, na anatarajiwa kurejea nchini kesho ili kuungana na timu katika maandalizi ya mwisho kuelekea pambano la Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga SC, linalotarajiwa kupigwa Oktoba 10.

“Ninaendelea vizuri na timu yetu, natarajia kurejea nchini kesho na baada ya hapo programu nyingine ya timu itaendelea. Naamini matokeo mazuri tutayapata katika siku hizi zinazokuja,” alisema Kasuru.

Chachu Kwenye Michuano ya Kimataifa

Mbali na Dabi ya Kariakoo, Kasuru aliongeza kuwa matokeo chanya ya Simba Queens yatakuwa chachu ya ushindi sio tu kwenye Ligi Kuu, bali pia katika michuano ya kimataifa ambayo Simba SC inashiriki mwezi huu.

“Mashindano ya Ngao ya Jamii kwa wanawake yataongeza morali na hamasa kwa Senior Team ili ifanye vizuri, sio kwenye Dabi pekee, bali hata kwenye michuano ya kimataifa inayotukabili mwezi huu,” alisisitiza.

Kwa sasa, mashabiki na benchi la fundi la Simba wanasubiri kwa hamu kurejea kwa timu hiyo kutoka Afrika Kusini kabla ya kuingia kambini kikamilifu kwa ajili ya kuikabili Yanga na kuendelea na mechi za kimataifa.

Simba Yafungwa Tena Sauzi, Sekhukhune 2-1 β€” Barker Ana Wiki Moja Kabla Ya Dabi De Reuk Aipigia Yanga Mkwara Mzito: “Tuko Tayari Kwa Dabi ya Kariakoo!”