Rushine atuma salamu Yanga
Simba SC

De Reuck na Kocha Barker Funguka Dabi ya Kariakoo: Simba Ipo Tayari!

Vardo October 5, 2026 8:01 pm

DAR ES SALAAM: Klabu ya Simba imerejea nchini ikitokea Afrika Kusini ilikoweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga. Mara baada ya kuwasili, beki na nahodha wa timu hiyo, Rushine De Reuck, pamoja na Kocha Mkuu Steve Barker wameweka wazi maandalizi yao kuelekea mpambano huo mzito.

Simba itakuwa mwenyeji wa dabi hiyo ya kwanza ya ligi msimu huu, inayotarajiwa kupigwa Oktoba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam—mchezo ambao tayari umeanza kupandisha joto la mashabiki wa soka nchini.

Kambi ya Afrika Kusini na Mipango ya Ushindi

Wekundu wa Msimbazi waliweka kambi katika Jiji la Polokwane, Afrika Kusini, ambapo walicheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu. Licha ya matokeo ya mechi hizo, kambi hiyo imeelezwa kuwa na mafanikio makubwa katika kujenga utulivu na mbinu za ushindi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Rushine De Reuck—ambaye anatarajiwa kuongoza jahazi hilo kutokana na nahodha mkuu Shomari Kapombe kuwa majeruhi—alisema kikosi kipo tayari na kina kiu ya kupata matokeo chanya pekee.

“Bila shaka tumepata muda mzuri wa kujiandaa na tupo tayari kwa mchezo huu. Tumekuwa na wakati mzuri kama timu, na hii itatupa faida kubwa. Tunajua tunakwenda kukutana na Yanga yenye ubora, lakini kuna hesabu tulizofanya tukiwa Afrika Kusini zitakazotupa matokeo wanayoyataka viongozi na mashabiki wetu. Tunahitaji ushindi ili kulinda heshima ya klabu,” alisema De Reuck.

Kocha Steve Barker Awatuliza Mashabiki

Kwa upande wake, Kocha Mkuu Steve Barker amewataka mashabiki wa Simba kutotiwa hofu na matokeo ya mechi za kirafiki walizopoteza nchini Afrika Kusini, kwani lengo kuu lilikuwa ni kujenga mfumo na stamina ya wachezaji.

“Hakuna sababu ya mashabiki wetu kufikiria kuhusu matokeo ya mechi za kirafiki kule Afrika Kusini. Kuna mambo ya msingi zaidi tulikuwa tunazingatia kuliko matokeo ya mwisho; tuna hesabu zetu,” alifafanua Barker.

“Kitu kinachonifurahisha ni namna wachezaji walivyojituma mazoezini. Tumerudi mapema ili kuendelea na maandalizi tukiwa hapa nyumbani, kila mmoja yupo sawa na tunataka kuonyesha kiwango cha tofauti.”

Dabi ya Kariakoo: Bodi ya Ligi Yaja na Teknolojia Mpya ya Gas Detector Vyumbani Lwandamina Afunguka Zito kuhusu Albert Kangwanda Yanga SC