Hemed Suleiman Morocco TRA United
Michezo Bongo

Kocha Morocco Afunguka Siri ya Kambi ya TRA United Zanzibar | Ligi Kuu Bara

Vardo October 5, 2026 10:33 am

Kocha Mkuu wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ameeleza kuwa kambi ya zaidi ya wiki moja iliyowekwa na kikosi hicho visiwani Zanzibar imekuwa na matokeo chanya zaidi katika kujenga utulivu wa wachezaji kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na chombo cha habari cha soka la bongo, Morocco alisema kuwa kambi hiyo imekuwa na manufaa makubwa, hasa katika kipindi hiki cha kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwani imewapa fursa ya kufanyia kazi upungufu uliojitokeza kwenye michezo iliyopita.

“Bado hatuna muunganiko mzuri wa kiuchezaji kwa maana ya safu yetu ya kujilinda na ile ya ushambuliaji. Tunafunga mabao lakini tunaruhusu pia; hiyo ndiyo kazi kubwa tuliyokuwa tunaifanyia mazoezini na maendeleo yetu ni mazuri,” alisema Morocco.

Ushindani Mkubwa Ligi Kuu Msimu wa 2026-2027

Morocco aliongeza kuwa kambi hiyo iliyoanza tangu Septemba 21, 2026, italeta matokeo mazuri uwanjani, ingawa alikiri kuwa ushindani wa msimu huu wa 2026-2027 ni mkubwa kutokana na kila timu kuingia uwanjani ikiwa na malengo madhubuti.

Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa—ambaye amewahi kuifundisha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) pamoja na vilabu vya Simba SC, Namungo FC, na Geita Gold—alijiunga rasmi na TRA United mnamo Septemba 10, 2026. Alichukua mikoba ya Mrundi Etienne Ndayiragije aliyeachana na timu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili Septemba 7, 2026.

Mwanzo Mpya Chini ya Morocco

Mwalimu wa awali, Ndayiragije, aliyejiunga na timu hiyo Novemba 16, 2025, akitokea Kenya Police FC (ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya msimu wa 2024-2025), aliacha TRA United ikiwa na mwenendo wa kusuasua. Katika mechi tano alizowaongoza msimu huu, alipata sare tatu na kufungwa mechi mbili, huku timu ikisalia nafasi ya 13 ikiwa na pointi tatu pekee na mabao matatu ya kufunga dhidi ya matano ya kufungwa.

Hata hivyo, Morocco ameanza safari yake vyema ndani ya TRA United. Katika mchezo wake wa kwanza tangu achukue mikoba hiyo, aliongoza timu kupata ushindi wa kwanza wa mabao 3-1 dhidi ya Pamba Jiji, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, mchezo uliochezwa Septemba 13, 2026.

Ally Kamwe Afunguka Mazito Kuelekea Dabi ya Yanga vs Simba | Ligi Kuu Abdulkarim Segeja Afunguka Sababu ya Kusaini Miezi 6 Kigamboni United