Simba vs Yanga / Dabi ya Kariakoo
Simba SC

Ahmed Ally: Dabi ya Kariakoo Ndiyo Vipimo Sahihi cha Simba | Simba vs Yanga

Vardo October 7, 2026 12:29 pm

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa mchezo ujao wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga utakuwa kipimo sahihi cha utimamu na ubora wa kikosi chao kwa msimu huu.

Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga SC siku ya Jumamosi, Oktoba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam—mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka nchini.

Akiuzungumzia mchezo huo, Ahmed ameeleza kuwa ingawa Simba ina kikosi imara na chenye ubora, bado kuna changamoto ndogo ya kujiamini kwa asilimia 100 kutokana na matokeo yasiyoridhisha dhidi ya Yanga katika mechi za hivi karibuni.

“Kujiamini kunakuja kutokana na hali ya wewe kuwa Simba; hilo pekee linatupa ujasiri. Lakini pia ubora uliopo sasa kwenye timu yetu unaongeza kujiamini zaidi kuelekea mchezo huu mgumu,” amesema Ahmed Ally.

Safari ya Kurejesha Hali ya Kujiamini

Ahmed alibainisha kuwa matumaini ya Wanasimba yalianza kurejea baada ya kupata sare mbili msimu uliopita, kisha kufuatiwa na ushindi wa Kombe la Muungano ambao uliongeza amani na imani kwa mashabiki na benchi la fundi. Matokeo hayo yaliwafanya Wanamsimba kuamini kuwa timu yao ilikuwa imetoka kwenye kipindi kigumu dhidi ya mtani wake.

Hata hivyo, kipigo cha hivi karibuni kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kilileta mitazamo tofauti. Wapo mashabiki walioona matokeo hayo kama sehemu ya mchezo, huku wengine wakianza kujiuliza kama timu hiyo imerejea tena kwenye wimbi la kutopata matokeo mbele ya Yanga.

Dakika 90 Kutoa Majibu ya Uteja

Meneja huyo amesisitiza kuwa Dabi ya Kariakoo ya Jumamosi hii haitakuwa tu mechi ya kusaka pointi tatu, bali ni fursa pekee ya kutoa majibu ya maswali yote yanayoulizwa na mashabiki.

“Yote kwa yote, mechi hii ya Jumamosi ni mechi inayokwenda kutoa majibu mengi sana. Itadhihirisha kama tumeshavunja uteja, kama tuna timu bora ya kushindana, na kama tuna uwezo wa kumfunga mpinzani wetu na kugombea ubingwa msimu huu. Ni mechi yenye majibu meza kuu ndani ya dakika zake 90,” alihitimisha Ahmed Ally.

Banana Zoro Funguka Mambo Mazito: Afya ya Mzee Zorro na Usiri wa Familia Lamine ni Silaha ya Barcelona Kwasasa