Dabi ya Kariakoo Simba na Yanga
Michezo Soka la Bongo

Dabi ya Kariakoo: Makocha wa Zamani wa Simba na Yanga Watabiri Bingwa, Robertinho na Nabi Watoa Siri Nzito!

Vardo October 10, 2026 8:52 am

Wakati presha ikizidi kupanda kuelekea mchezo mkubwa wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, makocha wa zamani wa vigogo hao wa soka la Tanzania wamegawanyika wazi kuhusu timu itakayoibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo.

Robertinho: “Natamani Simba ishinde, lakini Yanga ina kikosi bora”

Kocha wa zamani wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ameweka wazi hisia zake akisema anatamani kuona timu yake ya zamani ikishinda, ingawa anakiri kuwa Yanga ina kikosi imara na chenye uzoefu.

Robertinho amekumbushia machungu ya kufungwa mabao 5-1 dhidi ya Yanga mwaka 2023, akisisitiza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu sana kutokana na ubora na uzoefu wa wachezaji wa upande wa pili. “Simba akishinda nitafurahi sana… changamoto kubwa kwa Simba ni kwamba Yanga ina timu yenye uzoefu mkubwa na mechi za namna hii,” alisema Robertinho.

Nasreddine Nabi: “Yanga ina wachezaji wanaojuana na kujiamini”

Kwa upande wake, aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema hakuna mshindi wa wazi kwenye dabi hii kutokana na makocha wote wawili kufahamiana vizuri kiufundi. Nabi ameongeza kuwa ushindi wa Yanga kwenye Ngao ya Jamii utawafanya Simba kuja kwa kasi kubwa sana. “Yanga wana timu ya wachezaji wanaojuana na nimeona wanacheza kwa kujiamini sana,” alisema Nabi.

Takwimu zinaonyesha kuwa wakati Nabi akiwa Yanga, aliongoza timu hiyo kwenye mechi 9 za kimashindano dhidi ya Simba, akishinda 4, sare 3, na kupoteza 2, huku Robertinho akiongoza Simba kwenye dabi 3 tu (kushinda 1, sare 1, na kupoteza 1).

Mtazamo wa Hadimu wa Soka: Kibadeni na Mkwasa

Mkongwe na kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King’, amewataka wachezaji kuzingatia maelekezo ya makocha wao ili kuonyesha soka safi lenye burudani kwa mashabiki na kuweka mfano mzuri kwa vijana wadogo.

Naye Charles Mkwasa ‘Master’, kocha na nyota wa zamani wa Yanga, amesema dabi mara nyingi hutumia nguvu na mbio nyingi kuliko ufundi wa hali ya juu, akibainisha kuwa timu itakayopunguza makosa ndiyo itakayochukua ushindi leo.

Beno Kakolanya: Siri ya Ushindi na Tahadhari kwa Diarra na Kassali Kariakoo Dabi