Guinness Matchday KMC Complex
Michezo

Guinness Matchday, Kmc Complex Mashabiki Wa EPL, Dabi Ya Kariakoo Watawala

Vardo October 10, 2026 7:11 pm

Dimba la KMC Complex, lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, liligeuka kuwa kitovu cha burudani ya michezo baada ya kufurika kwa maelfu ya mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia hafla kubwa ya Guinness Matchday, iliyoleta msisimko wa kipekee wa Ligi Kuu ya England (EPL) na soka la ndani.

Hafla hiyo maalum iliwakutanisha wapenzi wa soka kutoka pande mbalimbali ili kufuatilia kwa karibu mechi za kusisimua za EPL, huku ikiwapa fursa adimu ya kujionea kwa macho yao kombe rasmi la ligi hiyo maarufu duniani na kupiga nalo picha za kumbukumbu.

Msisimko wa EPL na Dabi ya Kariakoo

Uwanja huo ulishuhudia shangwe kubwa wakati mashabiki wakifuatilia timu zao zilizokuwa zikicheza Ulaya. Arsenal iliibuka na ushindi mtamu wa mabao 2-1 dhidi ya Leeds United, wakati Chelsea ikiwanyoosha Bournemouth kwa mabao 5-1. Mbali na mechi hizo, msisimko ulipanda zaidi pale ambapo pambano kali la Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC lilipochukua nafasi na kuwa moja ya vivutio vikubwa vya siku hiyo.

Burudani haikuishia hapo, kwani mashabiki waliendelea kushuhudia mechi nyingine ya kibabe ya EPL kati ya Manchester United na Tottenham Hotspur, kabla ya kuhamia kwenye jukwaa la burudani ya muziki.

Mchanganyiko wa Soka na Muziki

Guinness Matchday ilifanikiwa kuunganisha mapenzi ya soka na burudani ya kizazi kipya, huku ikipambwa na burudani ya nguvu kutoka kwa magwiji wa muziki wa Bongo Fleva, Fid Q na Alikiba, jambo lililofanya tukio hili kuwa la kipekee na lisilosahaulika kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Dabi ya Kariakoo: Hali Halisi ya Uwanja wa Uhuru Masaa Machache Kabla ya Mchezo