BOSI SIMBA AOMBA VAR KWENYE DABI
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, amesema inahitajika VAR (Video Assistant Referee) kwa ajili ya kung’amua matukio tata ikiwemo penalti ambayo walipata wapinzani wao Yanga walipocheza nao Novemba 7. Hans Poppe ameongeza kwamba VAR hiyo itakuwa msaada mkubwa wa kutoa haki baada ya waamuzi wengi kuonekana kuwa na...
WACHEZAJI WA BARCELONA KUKATWA MSHAHARA
IMEELEZWA kuwa mabosi wa Klabu ya Barcelona inayoshiriki La Liga nchini Hispania ipo kwenye mpango wa kuwapunguzia asilimia 30 mshahara wachezaji wake wote wanaolipwa pesa ndefu ili kuepuka janga la kufilisika.Hali hiyo imefikia hapo kutokana na timu hiyo kupitia kwenye kipindi cha mpito hasa kwenye masuala ya malipo kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo limeyumbisha mambo mengi...
BEKI WA LIVERPOOL TRENT ALEXANDER NJE WIKI NNE
BEKI wa Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Trent Alexander-Arnold ameongezeka kwenye idadi ya wachezaji majeruhi ambao watakosekana ndani ya uwanja kwa kuwa yeye imeelezwa kuwa atakuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja. Beki huyo aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Uwanja wa Etihad kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na kwenye wiki nne hizo...
MASHABIKI RUKSA KUWAONA STARS KWA MKAPA
RASMI sasa mashabiki wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataruhusiwa kushuhudia mtanange kati ya Stars dhidi ya Tunisia ambao ni kwa ajili ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 nchini Cameroon.Stars ambayo ipo kundi J itaaendelea kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Tunisia Novemba 13 ikiwa ugenini ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa bila mashabiki kutokana na taarifa...
MWALIMU KASHASHA AIPA PONGEZI GLOBAL GROUP, AWATAJA WATATU WACHAPAKAZI
MCHAMBUZI nguli wa masuala ya soka nchini, kwenye kituo cha radio cha TBC Taifa, Mwalimu Alex Kashasha, amefunguka kuwa, hakuwahi kuhisi kama kampuni ya Global Publishers itakuwa na wigo mpana katika nyanja ya habari kama ambavyo amejionea mwenyewe. Kashasha ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 10-2020 alipotembelea ofisi za Global Publishers zIlizopo Sinza Mori Jijini Dar es salaam, inayomiliki magazeti ya...
CLATOUS CHAMA AITWA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA
NYOTA wa Klabu ya Simba, Clatous Chama ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Zambia ili akaitumike timu yake hiyo maarufu kama Chipolopolo.Kwa sasa timu ya Zambia ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu Afcon ambapo itamenyana na Botswana, Novemba 12 nchini Zambia.Kiungo huyo ambaye amekuwa kwenye ubora ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21 akiwa na pasi tano za...
SAMATTA KUIKOSA TUNISIA NOVEMBA 13
IMEELEZWA kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na timu ya Taifa ya Tunisia Novemba 13.Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji 27 walioitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.Kwa sasa Stars chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije imeweka kambi nchini Uturuki...
KAZE ABAINISHA MKAKATI NAMBA MOJA WA YANGA
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2020/21 ni kuendelea kupata pointi tatu kwenye mechi zote watakazocheza ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.Baada ya kumaliza Dar Dabi ya kwanza Novemba 7 kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa, hesabu yao inayofuata ni dhidi ya Namungo FC.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa...
JOSE MOURINHO ATAJA KIKOSI CHAKE BORA CHA MUDA WOTE, DROGBA NDANI
JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Spurs ametaja orodha ya wachezaji wake 11 bora wa muda wote ambao amewahi kufanya nao kazi huku nane kati ya hao akiwataja aliofanya nao kazi ndani ya Klabu ya Chelsea huku majina ya nyota kama Paul Pogba, Sergio Ramos na Zlatan Ibrahimovic yakikosekana. Mourinho alikuwa ndani ya Stamford Bridge mwaka 2004 na aliweza kufanikiwa kutwaa...
HESABU ZA SIMBA KWA SASA NI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.Msimu uliopita Simba ilipokuwa chini ya Patrick Aussems iliishia hatua ya awali kwa kutolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini jambo ambalo lilisababisha kibarua cha kocha huyo ambaye aliifikisha hatua ya robo fainali timu...